nadharia ya sarufi zalishi
Katika
kazi hii tumejadili nadharia ya sarufi zalishi ambapo tumeangalia msingi wa
nadharia hii pamoja na dhana zake,pia tathmini yetu kuhusu nadhalia hii. Lakini
kabla ya kuijadili nadharia hii tutaanza na kutoa maana ya istilai mbalimbali
ambazo zinapatikana katika kazi hii kwa mujibu wa wataalam mbalimbali.
Massamba,
(2009) anasema kuwa, nadharia ni taratibu , kanuni na misingi ambayo imejengwa
katika muundo wa kimawazo kwa madhumuni ya kutumiwa kama kielelezo cha kueleza
jambo.
Wafula
na Njogu (2007) wanasema, nadharia ni jumla ya maelekezo yanayomsaidia msomaji
au mhakiki kuifahamu kazi ya fasihi kwa kufuata utaratibu maalumu.
Hivyobasi,nadharia
ni mawazo au mwongozo unaomsaidia mtu kueleza kutatua au kueleza jambo fulani.
Kihore
(2005) anasema, sarufi ni sayansi ya muundo wa lugha pamoja na sheria, kanuni
na matumizi yake ambayo kwa kawaida hukubalika kwa watumiaji wake.
Massamba
na wenzake (1999) wanaeleza kuwa, sarufi ni kanuni na sheria au taratibu za
uchambuzi zinazotawala lugha.
Hivyobasi,
sarufi ni taaluma ya uchambuzi wa lugha inayojumuisha viwango vyote vya
uchambuzi yaani kiwango cha umbo, kiwango cha sauti, kiwango cha miundo na
kiwango cha maana.
Baada
ya kuangalia maana ya dhana hizi kutoka kwa
wataalam mbalimbali.
Nadharia
sarufi zalishi iliasisiwa na mwanaisimu Noam Chomsky (1928) ambaye alichapisha
kitabu Syntactic structures mwaka (1957) ambapo katika kitabu hiki alizua dhana
ya sarufi zalishi, ambayo ilileta mapinduzi ya msingi katika taaluma ya isimu.
Mawazo ya Chomsky yalidhihirisha kuwa mbinu za uchanganuzi wa sentensi
zilizotumika hapo awali hazikuwa toshelevu, hivyo sarufi zalishi ilizuka
kutokana na kasoro za sarufi miundo katika uchanganuzi wa lugha.(Matinde, 2o12)
Chomsky,
amewasilisha mtazamo wa Sintaksia unaotambuliwa kama Sarufi Zalishi.Katika kazi hiyo,Chomsky alikusudia
kukuza fafanuzi mwafaka za hali ya sintaksia ya lugha mbalimbali,yaani jinsi
lugha mahususi zinavyounganisha maneno kuunda sentensi.Vile vile kazi hiyo
ilidhamiria kukuza nadharia ya kijumla ya sintaksia inayobainisha ni mambo yapi
ya kijumla yanayopatikana katika lugha mbali mbali na jinsi gani masuala hayo
yanavyotofautiana katika uwanja huu wa sintaksia.
Msingi
wa nadharia ya sarufi zalishi ulijikita katika uundaji wa nadharia ambayo
ingeeleza namna lugha hutumiwa na watumiaji wake hasa kwa kutazama namna
wanavyotumia kanuni chache zilizopo katika lugha yao kuzalisha sentensi nyingi
na zisizo na kikomo, katika kurejerea hali mbalimbali, ingawa sentensi hizo
zinaweza kuwa sahihi au zisizo sahihi.
(
Matinde, 2012)
Dhana za msingi za nadharia sarufi zalishi;
Umilisi, huu ni ujuzi alionao mjua lugha kuhusu lugha yake. Ni ujuzi
alio nao mjua lugha ambao upo katika ubongo wake. Ujuzi huo huhusu kanuni
zinazotawala lugha hiyo husika. Ujuzi huu humwezesha kutambua sentensi sahihi,
zisizo sahihi na kupambanua sentensi zenye utata. Ujuzi huo humwezesha kupuuza
makosa ya kiutendaji katika mazungumzo kama vile kuteleza kwa ulimi, na
kukatisha sentensi.
Chomsky
anaeleza kuwa mtu anapojifunza lugha
huanzia na umilisi (ujuzi) na anaendelea kudai kuwa kwa kiasi kikubwa umilisi
wanaokuwa nao wazawa wa lugha moja hufanana na hii ndiyo inayowafanya waelewane
katika mazungumzo yao kwamba mzungumzaji anasema kile anachotaka kusema na
msikilizaji anaelewa kile kilichosemwa na msikilizaji.(Rubanza,2003)
Umilisi
humwezesha mzawa wa lugha:
Ø
Kuijua miundo ya sentensi
katika lugha yake mfano mmilisi wa lugha ya kiswahili lazima ajue muundo wa
sentensi za kiswahili kuwa unaanza na nomino,ukifuatiwa na kitenzi na kuishia
na kielezi.
Mfano: Baba anaongea
na mjomba. Juma
amekwenda sokoni.
Kwa hiyo mmlisi wa lugha hawezi kuchanganya muundo huu wa sentensi za
kiswahili kwa kusema;
Mfano: Amekwenda Juma
sokoni. Shambani analima baba.
Kwa hiyo, kulingana na muundo wa
sentensi za kiswahili, muundo wa sentensi zilizopo katika mfano wa pili si
sahihi kwani zimekiuka sintaksia ya lugha Kiswahili.
Ø kutambua
sentensi sahihi na mbazo si sahihi mfano:
Hamis ni kijana mpole (Sahihi)
Mtundu mtoto ni wako (si
sahihi)
Ø Kutunga
sentensi nyingi zenye urefu wowote:
Kijana
mpole na mstaarabu uliyeonana nae jana, nimekutana nae leo asubuhi amekamatwa
na polisi kwa tuhuma za ujambazi.
Ø kutambua
sentensi zenye utata, mfano;
Baba Joni amefika.
Nyumbani kwao kuna mbuzi
Ø kutambua sentensi zenye maana sawa.
Mfano;
Watoto wapo uwanjani wanacheza
mpira.
Mpira unachezwa na watoto uwanjani.
Ø kutambua aina mbalimbali za sentensi katika
lugha yake,
mfano;
Leo ni sikukuu ya mashujaa
(sentensi arifu).
Njoo hapa! (sentensi amrishi)
Umenunua kalamu ngapi? (sentensi
ulizi)
Kumbe umerudi! (sentensi mshangao)
Hansi angelisoma kwa bidii angelifaulu.
(sentensi shurutia).
Hivyo mmilisi wa
lugha huweza kuelewa sentensi hizi zinataka nini.
Ø kutambua
sentensi zenye maana na zile zisizo na maana.
Mfano;
·
Kitabu anasoma
mwanafunzi.
·
Mwanafunzi anasoma
kitabu.
Mmilisi wa lugha
huweza kuelewa kuwa sentensi ya kwanza ni sahihi, lakini sentensi ya pili si
sahihi.
Dhana nyingine ya msingi katika nadharia ya sarufi zalishi ni utendaji,
utendaji ni utumiaji wa lugha katika mazingira
halisi ambao huweza kuathiri maana za maneno kulingana na matumizi yake au mambo yanayomhusu mzungumzaji mwenyewe kama
vile kutokuwa makini au kukosa kumbukumbu, kuongea akiwa amekasirika, kasoro za
ala za sauti kamavile mapengo, kigugumizi na kadharika. Utendaji ni usemaji na
utumizi wa ujuzi wa mzawa wa lugha katika kutumia lugha yake ndani ya muktadha
mahususi, mtumiaji wa lugha huweza kuitumia lugha kulingana na mazingira
aliyopo. Matumizi ya lugha huzingatia muktadha, wahusika, jinsia, utamaduni na
mada ya mazungumzo. (Yule, G. 1997).
Mfano:
·
Muktadha:
Muktadha wa stendi -
Kula vichwa.
Muktadha wa hotelini -
nipe wali kuku.
Muktadha wa kanisani - Bwana awe nanyi.
·
Wahusika
matumizi ya
lugha huzingatia wahusika, kuna matumizi tofauti ya lugha kutegemeana na kundi
la wahusika. Kundi la rika moja hutumia lugha inayofanana mfano kundi la vijana
hutumia misemo kama;
Twende tukale bata
Leo Unaniachaje?
Kundi la watu
wenye rika tofauti huwa na matumizi tofauti ya lugha.
Mfano;
Mzazi na mtoto
Mzazi:
Mwanangu niletee kikoi changu.
Mtoto: Sawa mama.
Mwajiri na
mwajiriwa.
Mwajiri
: Leta faili la madai.
Mwajiriwa: sawa mkuu.
Mada ya
mazungumzo
Mada za
mazungumzo zipo nyingi, Kuna mada za kijamii, kwa mfano ndoa, unyago, mapenzi,
kifo, matanga, burudani na muziki Kuna
mada za kibiashara kwa mfano bidhaa, kodi, vibali, fedha, hasara na faida. Kwa hiyo, ili mazungumzo yaweze kwenda vizuri,
wazungumzaji wanatakiwa kuzingatia mada husika.
Mfano:
wafanyabiashara
Mzigo mpya umeingia.
Nauza vocha kwa bei ya jumla.
Mada ya kilimo
Mbolea ya ruzuku bado
haijaletwa.
Mwaka huu nitawahi
kupalilia shamba.
Dhana nyingine
ya nadharia ya sarufi zalishi ni umbo la ndani, umbo hili hujitokeza katika
sentensi kabla ya sentensi hiyo kufanyiwa mageuzi yoyote. Umbo la ndani hubeba
maana kamili ya tungo na vipashio vya tungo hubainika bayana kwani huwa
havijafanyiwa mageuzi yoyote.
Mfano sentensi
zifuatazo zipo katika umbo la ndani
Amina piga mtoto kila siku
Shida anunua chumvi kwa
mangi
Mama enda shambani asubuhi.
Mpendi wangu amerudi
Umbo la nje,
umbo hili hutokea baada ya umbo la ndani kufanyiwa mageuzi muhimu hadi kufikia
kiwango cha usemaji sahihi na unaokubalika. Umbo la nje hudhihirika kimatamshi
na kiothografia, yani umbo hili hutamkika na kuandikika.
Mfano; Amina humpiga mtoto kila siku
Shida amenunua chumvi kwa
Mangi.
Mama ameenda shambani asubuhi.
Mpenzi wangu amerudi.
Dhana ya mwisho
ya sarufi zarufi ni uchamko, chamko ni
utaratibu wa kutumia sheria fulani ambazo huweza kutumika mara kwa mara katika
kuunda sentensi ambazo zina urefu usio na kikomo . uchamko hutokana na sentensi
zaidi ya moja kupachikwa katika Sentensi ile ya kwanza ili kuunda sentensi moja
isiyo na kikomo, pia hutumia kanuni chache kutunga sentensi nyingi zisizo na
kikomo. Uchamko umegawanyika katika sehemu mbili yaani utegemezi na
uambatanishaji.
Utegemezi
Ni uchamko ambao
hutokana na hali ya kuwepo au kutokuwepo kipashio kimoja cha kiisimu ambacho
kinategemea uwepo wa kipashio kingine. Utegemezi hutambulishwa na maneno kama
vile; ili, kwamba, kama na kuwa. (Matinde, 2012)
Mfano; Ambakisye alijua kuwa Ndope anafahamu
kuwa shule itafunga kesho.
Asha anajua kuwa mimi najua kuwa
atafaulu mtihani.
Uambatanishaji.
Ni aina ya
uchamko ambao hudhihirishwa na uambatishaji wa sentensi sahili mbili au zaidi.
Kwahiyo, huu ni uchamko ambao hutokana na sentensi ambatano.
Mfano; Shangazi anapika, mama anaandaa chakula na
baba anakula.






















Baba anakula
Kama
ilivyo kwa nadharia zingine nadharia hii pia ina ubora na udhaifu wake.
Ubora
wa nadharia hii.
·
Imeweza kuonesha
umilisi alionao binadamu katika lugha yake, kuwa anaweza kuzalisha tungo au
sentensi mbalimbali kwa kutumia kanuni chache zilizopo katika lugha
yake.Umilisi huo humsaidia mtumiaji wa lugha kuunda sentensi hizo hata kama
hajui kusoma na kuandika.
·
Pia nadharia hii
inaonesha kuwa kila mzungumzaji wa lugha huzifahamu vizuri kanuni chache
zilizopo katika lugha yake na kuzitumia kanuni hizi katika kuwasiliana na jamii
inayomzunguka.
·
Vilevile nadharia hii
ya sarufi zalishi imeweza kuonesha kuwa binadamu anao uwezo wa kufafanua kipi
ni sahihi na kipi sio sahihi katika uteuzi wa maneno wakati wa uzungumzaji.
·
Nadharia hii
inamchukulia binadamu kama kiumbe chenye uwezo endelevu wa kuzalisha sentensi
ambayo inaweza kueleweka kwa jamii inayomzunguka.
·
Pia nadharia
inatuonesha kwamba upo uhusiano mkubwa kati ya akili, kufikili na lugha.Hususan
katika dhana ya utendaji mtumiaji wa lugha anatakiwa kutumia akili anapoteua
lugha ya kutumia ili kuendana nas muktadha.
Udhaifu
wa nadharia hii.
·
Inafafanua namna au
jinsi watu wanavyozungumza lugha na sio kuwaeleza wazungumze vipoi lugha hiyo.
·
Haitilii mkazo
mabadiliko katika lugha hata kama yapo.
·
Vipengele kama umbo la
ndani na umbo la nje vinaweza kumchanganya mtu anaejifunza lugha.
Hivyo
ni kweli kwamba nadharia ya sarufi zalishi imeleta mapinduzi makubwa katika
taaluma ya sarufi miundo.
Kabisa,lugha ya kiswahili kitukuzwe
ReplyDeleteKiswahili kitukuzwe duniani
Deletelugha kitukuke
ReplyDeleteNina swali,huku ukitoa mifano,fafanua majukumu ya nomino katika nadharia ya semantiki zalishi
ReplyDeletefafanua jinsi ferdinand de saussure alivyochangiakatika taaluma ya isimu
ReplyDeleteNashukuru kwa hii dondoo ya sarufi zalishi. Je ni zipi sheria za uchamko?
ReplyDeleteDhana ya mofimu kabla ya sarufi zalishi
ReplyDeleteNina swali
ReplyDeleteSifa za mofimu kabla ya sarufi zalishi ni zipi?
ReplyDelete