nadharia ya sarufi zalishi
Katika kazi hii tumejadili nadharia ya sarufi zalishi ambapo tumeangalia msingi wa nadharia hii pamoja na dhana zake,pia tathmini yetu kuhusu nadhalia hii. Lakini kabla ya kuijadili nadharia hii tutaanza na kutoa maana ya istilai mbalimbali ambazo zinapatikana katika kazi hii kwa mujibu wa wataalam mbalimbali. Massamba, (2009) anasema kuwa, nadharia ni taratibu , kanuni na misingi ambayo imejengwa katika muundo wa kimawazo kwa madhumuni ya kutumiwa kama kielelezo cha kueleza jambo. Wafula na Njogu (2007) wanasema, nadharia ni jumla ya maelekezo yanayomsaidia msomaji au mhakiki kuifahamu kazi ya fasihi kwa kufuata utaratibu maalumu. Hivyobasi,nadharia ni mawazo au mwongozo unaomsaidia mtu kueleza kutatua au kueleza jambo fulani. Kihore (2005) anasema, sarufi ni sayansi ya muundo wa lugha pamoja na sheria, kanuni na matumizi yake ambayo kwa kawaida hukubalika kwa watumiaji wake. Massamba na wenzake (1999) wanaeleza kuwa, sarufi ni kanuni na sheria au taratibu za uchambuzi ...