maana ya sintaksia,uhusiano wa sintaksia na matawi mengine,malengo ya sintaksia au isimu miundo, vipashio vya lugha ni vipi?,
TUKI (1990) wanaeleza na wanafasili dhana hii ya sintaksia au isimu miundo kuwa ni tawi la sarufi linaloshughulikia uchanganuzi wa mpangilio na uhusiano wa vipashio katika kila sentensi. Habwe na Karanja (2004) wanapambanua dhana hiii ya “sintaksia ni utanzu wa isimu unaoshughulikia muundo wa sentensi na elementi nyingine zinazounda sentensi kama vile kategoria za maneno, vikundi na vishazi” Radford (1981) anasema isimu miundo au sintaksia ni taaluma inayojishughulisha na namna maneno yanavyoweza kupangwa pamoja kutoa muundo wa sentensi. Radford anaangalia jinsi neno moja linavyoweza kujihusisha na neno lingine na kutathmini muundo uliosahihi. Dhana ya sintaksia ni utanzu wa sarufi unaojishughulisha na uchanganuzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipashio vyake.( Massamba na wenzake (2001) Sintaksi (au sarufi miundo / muundo ) ni tawi la isimu au taaluma ya sarufi inayoshughulikia namna ambavyo vikundi vya maneno na sentensi mbalimbali zinajeng