Jamii lugh,ULUMBI,Msingi ya kutumia lugha,Msingi wa kutumia mahali,Msingi wa makubaliano wa kimazoea,Aina za jamii lugha,jamii lugha uwili,ulumbi, na sababu za ulumbi pamoja na matatizo yake.Diagrosia ni nini.
.
JAMII LUGHA MBALIMBALI
Dhana ya jamiilugha
Kwa mujibu wa Mekacha (2011) dhana ya jamii lugha imetafsiriwa
kwa mitazamo mbalimbali, hata hivyo wataalamu wengi wanakubaliana na maana ya
jumla kuwa jamii lugha ni watumiaji wa lugha wanaoishi katika eneo moja ambao
hubainishwa kwa mahusiano yao ya kuendelea kutumia aina fulani ya lugha tofauti
na watumiaji wengine wa lugha hiyohiyo. Licha ya fasili hii kuonekana kuwa ni
rahisi kueleweka, bado ina utata katika kupata data wakati wa uainishaji wa
wazungumzaji wake na uchanganuzi wa data za isimujamii. Utata huu unajibainisha katika mambo yafuatayo;
i.
Kujua mahali ambapo mipaka ya watumiaji wa lugha inaanzia na kuishia na
kama inawezekana kukawa na mipaka ya eneo moja la jamii lugha isiyoingiliana na
mipaka ya eneo lingine
ii.
Uwezekano wa wazungumzaji wa lugha katika jamii lugha moja, kuzungumza
lugha moja au zaidi. Je, wanatumia lahaja, lugha sanifu, misimu, lafudhi au
wanatumia lugha zote?
iii.
Vigezo vinavyotumika kuwabaini au kuwaainisha watumiaji wanaopatikana
katika jamii lugha moja na kuwafanya waonekane kuwa wa jamiilugha husika.
Maswali haya na mengine mengi yanaifanya tafsiri ya dhana
ya jamiilugha ionekane kuwa ni tata kinadharia na kiutendaji. Tutatumia misingi
mitatu ili kuifahamu dhana ya jamiilugha:
i.
Msingi wa kutumia lugha
Imezoeleka katika jamii nyingi lugha kutumika kama nembo
ya jamii fulani ambapo watu wanaotoka au wanaopatikana katika jamii fulani
hutambulishwa kwa lugha yao. Mfano tunaweza kupata lugha ya Kiswahili
(Waswahili), Kichaga (Wachaga), Kiingereza (Waingereza), Kijaluo (Wajaluo),
Kikalenji (Wakalenji) nakadhalika.
Katika utambulisho huu jamii au taifa linalotumia lugha
moja ndilo linalopewa lugha moja. Kunapokuwa na matumizi ya lugha zaidi ya moja
taifa au jamii husika haitambulishwi kwa Lugha, kwa mfano hutuwezi kuwa na
jamiilugha ya Watanzania, Wakenya, Waghana nakadhalika. Jamii hizi huwa ni
muktadha halisi wa matumizi ya lugha na si mtu mmojammoja kwa vile lugha ni
mali ya jamii.
Hii ni kusema, Jamiilugha hujidhihirisha katika
mawasiliano ambayo hufanikiwa katika misingi ifuatayo;
Ø
Kuelewana kwa wazungumzaji wa lugha miongoni mwao kunatokana na wazungumzaji
wenyewe kuwa ni zao la jamii moja
Ø
Watumiaji wa jamiilugha moja huelewana kiurahisi kwakuwa wanazielewa kanuni
na taratibu za mawasiliano zinazotumiwa na watumiaji lugha wote
Ø
Wazungumzaji wa lugha hiyo huwa na ujuzi na uzoefu wa muda mrefu wa kutumia
lugha hiyo kwa nia ya kurithishana.
Kwa mantiki hii, lugha ndio inayojiwekea mipaka ya
jamiilugha. Mipaka huanzia na kuishia mahali lugha inapoishia. Tatizo la mtazamo huu ni kuwa kwanza, kuwepo kwa baadhi ya watu kuanza
kutumia lahaja tofauti, Pili kunakuwa na matumizi ya lugha zaidi ya moja na
hivyo kuwa vigumu kupata jamiilugha kirahisi kwasababu kunapotokea jamii zaidi
ya moja kila jamii hujiona bora kuliko nyingine.
ii.
Msingi wa kutumia mahali/Eneo
Watu wanaounda jamiilugha moja wanakaa katika eneo moja
lenye mipaka mahsusi ya kijeografia. Wanassosholojia hutumia msingi wa mahali katika
kubaini jamiilugha. Huamini katika msingi kuwa, watu wanapokuwa katika eneo
moja kwa muda mrefu hujiundia kanuni na taratibu zao za namna ya kuishi, yaani
mila na desturi. Watu hawa hujiwekea mipaka yao ili kujitofautisha na jamii
nyingine, mipaka hii yawezakuwa milima, mabonde, mito, misitu minene
nakadhalika. Mipaka hii ya kijeografia huheshimiwa daima na kurithishwa kutoka
kizazi kimoja hadi kingine. Hivyo, ili kujua jamiilugha wataalamu wa lugha
hawana budi kutumia misingi ya mahali mahali na lugha kuibaini jamiilugha
kwakuwa ni vitu vinavyotegrmeana na kukamilishana.
iii.
Msingi wa makubaliano wa
kimazoea.
Ni msingi unaohusu jamiilugha
ndogondogo ndani ya jamiilugha kubwa katika eneo fulani. Jamiilugha hizi zaweza
kuwa za wafanyakazi wa kampuni fulani, wanafunzi, wanachuo, wafanyabiashara,
vijana, jinsia fulani nk. Msingi wa makubaliano ya usemaji unatokana na mazoea
ya muda mrefu kutokana na kuwa pamoja katika shughuli au mahali fulani. Tatizo
la jamiilugha za aina hii ni utata katika kupata idadi halisi ya jamiilugha
kutokana na kukosa ukomo. Hii inatokana na ukosefu wa mipaka dhahiri ya
jamiilugha moja na nyingine kwa kuwa mtu mmoja anaweza kujibainisha katika
jamiilugha zaidi ya moja. Mfano, mtu kuwa mfanyabiashara, mwanafunzi na
vilevile mfanyakazi wa bandarini. Msingi huu unaelekea kuwa si imara.
AINA
AU MAKUNDI YA JAMIILUGHA
1.
Jamiilugha zinazotumia lugha
moja
Ikiwa jamiilugha inatumia lugha
moja, basi jamiilugha hiyo inasemekana kuwa yenye kutumia lugha moja
(Monolingual speech community). Lugha hii hutumika katika maeneo yote ya
matumiazi ya lugha, maeneo rasmi ya utawala na serikali na yasiyo rasmi ya
matumizi ya lugha kama vile majumbani katika kiwango cha familia na mtu na mtu.
Wanajamii wote wandhaniwa kuielewa na kuitumia lugha husika kiufasaha katika
shughuli zao za kila siku.
Hata hivyo, katika karne ya leo
ambapo kuna maingiliano na mawasiliano bora zaidi mingoni mwa wanajamii duniani
ni vigumu kupata jamiilugha yenye kutumia lugha moja tu katika mawasiliano
yake. Ugumu huu unatokana na maingiliano kupitia njia mbalimbali kama uhamiaji,
utalii, elimu, dini, ndoa, ukimbizi, mawasiliano ya kimtandao nk.
Vilevile hata katika jamiilugha
yenye kutumia lugha moja bado kunaweza kutokea suala la tofauti za kilahaja.
Kwa upande mwingine watumiaji lugha wa mipakani hulazimika kujifunza lugha
nyingine zaidi kutokana maingiliano ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni na watu
kutoka katika jamiilugha wanayopakana nayo. Hii inawafanya wawe na lugha mbili
tofauti (jamiilugha uwili) kwa wakati mmoja..
Kimsingi dhana ya jamiilugha
inayotumia lugha mojailikuwepo kwa Tanzania kabla ya ujio wa wakoloni ambapo
kila jamii ilitumia lugha moja. Hivyo, kulikuwa na taifa la wahehe, wachaga,
wasukuma nk. Baada ya ujio wa wakoloni mataifa asilia yakawa chini ya utawala
mmoja. hivyo kukawa na mataifa makubwa zaidi kama ya Kenya, Tanzania na Uganda.
Hapo ndipo muingiliano ukawa mpana zaidi.
2.
Jamiilugha Uwili
Ikitokea katika jamii kuwa na
matumizi ya lugha mbili kwa wakati mmoja tunaweza kusema jamii husika ni
jamiilugha uwili. Kigezo kinachotumika ni idadi ya lugha zinazotumika.
Inawezekana kupata jamiilugha uwili katika mazingira ya Tanzania ambapo watu
wanaweza kuzungumza lugha ya Kiswahili na wakati huohuo wanazungumza lugha
mojawapo kati ya lugha za asili. Hata hivyo, kutokana na maendeleo ya sayansi
na teknolojia, mtu mmojammoja wanajua lugha zaidi ya mbili. Kiswahili, Kiingereza/
Kifaransa, Lugha ya/za asili nk.
3.
Jamiilugha Ulumbi
Katika mzingira ya kawaida kwa
watanzania kuna wakati wazungumzaji humudu lugha zaidi ya mbili. Mfano, mtu
anaweza kuzungungumza lugha moja au zaidi kati ya lugha za asili, Kiswahili na
lugha moja au zaidi. Mfano, anaweza kujua lugha ya Kinyakyusa, Kisafwa,
Kiswahili na Kiingereza hivyo kujua lugha nne. Mwingine anaweza kujua lugha
moja ya asili mfano Kisukuma, Kigogo na Kiswahili tu na akawa anajua lugha tatu
nk. Hivyo, idadi ya lugha katika jamiilugha ulumbi hutofautiana kati ya mtu na
mtu na jamiilugha na jamiilugha. Vilevile ikumbukwe kuwa kiwango cha umahiri
katika lugha anazojua mzungumzaji si lazima kiwe sawa. Kuna atamudu vizuri
zaidi lugha fulani ikilinganishwa na nyingine.
Sababu
za Kutokea Ulumbi
Ulumbi katika jamiilugha
inasemekana kuwa unasababishwa na mambo ya ndani ya jamii yenyewe na mambo
yanayotoka nje ya jamii. Kwa ujumla mambo hayo ni pamoja na uhamiaji,
ukimbizi, ukoloni, biashara, elimu, dini, mipaka ya kimataifa, Nguvu za dola,
teknolojia ya habari na mawasiliano, nguvu [kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni]
nk. Ieleweke kwamba sababu za kutokea kwa ulumbi hutofautiana kati ya jamii na
jamii na msemaji mmoja na mwingine.
Matatizo
ya Jamiilugha Ulumbi
Tatizo la kuteua lugha ya kutumia
kitaifa kati ya lugha zinazotumika. Mfano, kupata lugha ya taifa, lugha ya
kufundishia na lugha rasmi. Kila jamiilugha inaweza kuwa na nguvu kimatumizi au
kwa idadi ya wazungumzaji kiasi cha kutaka kuteuliwa na hivyo kuwa vigumu
kupata lugha kiurahisi.
Hata hivyo, inashauriwa kuwa
uteuzi wa lugha kitaifa unapaswa kufanyika kwa uangalifu sana kwa kushirikisha
makundi mbalimbali ya kijamii ili kuepuka minyukano ya kimaslahi miongoni mwa
wanajamii.
Vilevile ulumbi unaweza
kusababisha ukosefu wa umoja na mshikamano miongoni mwa wanajamii kwa vile
kunakuwa jamii zinazojibainisha katika lugha na kila jamii inakuwa na utamaduni
wake na hata mazingira yake.
MATUMIZI
YA LUGHA
Katika kipengele hiki
tunatarajia kuchunguza jinsi matumizi ya lugha yanavyojibainisha miongoni mwa
watumialugha na jamiilugha. Ni kwa nini lugha hutumika tofautitofauti kati ya
jamii moja na nyingine.
Sababu
za kutofautiana kwa matumizi ya lugha:
Umri, elimu, jinsia, dini,
matabaka [kisiasa, kiuchumi, kijamii], makabila, jiografia, nk.
Makundi
ya lugha za Tanzania
Tanzania ni nchi inayoonekana
kama eneo la makutano ya makundi ya lugha za asili katika Bara la Afrika.
Makundi haya ni Naija-Kongo (Bantu), Nailosahara, Afroasia (kikushitiki) na Kikhoisani.
Haya ni makundi ya msingi.
Nailosahara
Ni kundi lingine la lugha
ambalo asili yake ni Afrika ya Kaskazini Misri, Ethiopia na Sudani. Mfano wa
lugha za kundi hili Tanzania ni Kimasai
Afro-Asia
Ni kundi kubwa lilizaa kundi la kushiti ambalo
linajumuisha lugha kama Iraqw[kimbulu] 500,000 na lugha nyingine za Burunge,
Alangwa,Gorowa na Ma’a (Mbugu) zina jumla ya wazungumzaji 40,000. Sifa moja
kubwa ya lugha hizi ni sauti ya mkwaruzo kooni inayodhihirisha kuwa asili yake
ni Uarabuni.
Khoisani
Asili yake ni Afrika kusini. Mfano wa lugha TZ
ni Kisandawe na Kihazabe . Sifa kubwa ya lugha hii ni konsonanti za kukisi.
Bantu
Hili ni
kundi linatokana na kundi la Benue Kongo ambalo lilitokana na kundi la
Naija-kongo.Kundi hili linalojumuisha lugha nyingi zaidi pamoja wa wazungumzaji
nchini Tanzania. Linahusisha lugha kama vile Kisukuma, kichaga, kinyakyusa,
kiha nk.
Pamoja na
kuwepo kwa makundi haya, bado kuna matumizi ya lugha nyingine za kigeni kama
vile Kingereza, Kilatini, Kiarabu, Kifaransa, nk ingawa kwa viwango vidogo.
Diaglosia
Katika
jamii hutokea wakati mwingine lugha mbili kutumika, moja kutumika matika
mazungumzo ya kawaida katika familia, mtu na mtu wakati lugha nyingine hutumika
katika shughuri lasmi kama elimu mahakama, biashara, bunge nk. Vilevile inaweza
kutokea lugha moja kuwa na lahaja tofauti ambapo kunakuwa na lahaja ambayo
inatumika katika mawasiliano ya kawaida ilihali lahaja nyingine hutumika katika
mawasiliano rasmi. Lugha ua lahaja inayotumika katika mawasiliano ya kawaida
hupewa mhadhi ndogo C na inayopewa matumizi katika shughuri rasmi hupewa hadhi
ya juu J. kunapokuwa na mahusiano ya namna hii tunasema kuna Diaglosia
(kifaransa “diglossie”).
MAMBO
YANAYOJIPAMBANUA KATIKA DIAGLOSIA
a.
Uamilifu
Lugha au lahaja J hutumika
zaidi ikilinganishwa na lugha au lahaja C. Hii inatokana na kupewa majukumu
mengi zaidi mfano kaika elimu, mahakama, biashara, dini, mahusiano ya kimataifa
nk. Ni lugha inayoeleweka na kutumika na watu wengi zaidi ikilinganishwa na
lugha ua lahaja C. Wageni wanapotaka kujifunza hupenda kujifunza lugha J.
Vilevile maarifa mengi huwa katika Lugha au lahaja J ingawa ufafanuzi wake
waweza kufanyika katika lugha au lahaja C.
b.
Umaarufu
Watumiaji wa lugha huiona lugha
au lahaja J kuwa ni bora na maarufu zaidi kuliko C. Matokeo yake watu wengi
zaidi hujifunza na kutumia J. mfano, watu watataka kusikiliza nyimbo, filamu,
mashairi katika J hata kama hawaelewi ilikinganishwa na katika C. Vilevile
katika dini lugha C hutumika zaidi. Mfano Kiarabu, Kiswahili nk.
c.
Mapokeo katika maandishi
Jamii huamini kuwa lugha iliyo
katika maandishi ndiyo kiwakilisho sahihi cha lugha J. Hata tabaka la watumia
lugha J huamini hivyo. Matokeo yake lugha J hutukuzwa wakati C hupuuzwa. J
yaweza kuwa ya kizazi kilichopita au kilichopo
mfano mashairi, dini, falsafa, sheria, sayansi nk.
d.
Ujifunzaji Lugha
Katika kiwangoi cha familia
watu hutumia lugha C. Watoto wanapowasiliana wao kwa wao au na wazazi hutumia
Lugha C. Hata hivyo, katika shughuri rasmi kama vile elimu, mahakama, redioni
lugha J hutumika. Kanuni na miiko ya sarufi ya lugha J hufundishwa darasani
wakati lugha C hufundishwa kimapokeo/kwa kurithishwa.
e.
Usanifishaji
Lugha J imefanyiwa tafiti nyingi zaidi kuhusu
sarufi, msamiati, mitindo, otografia nk na miiko yake.Matokeo yake Lugha J inakuwa imesanifishwa na otografia
yake haibadiliki ingawa maana yaweza kubadilika katika muktadha fulani.
f.
Msamiati
Kunakuwa na mwingiliano mkubwa
wa msamiati kati ya lugha J na C. Hata hivyo, lugha J ina msamiati mwingi zaidi
wa kiufundi na kigeni ambao unakosa visawe katika J. Vilevile msamiati katika
lugha C mwingi sio rasmi. Kwa mifano;
Mother mum
Cigarette fag
Police officer cop
Steal pinch
Children kids
g.
Sarufi
Sarufi ya lugha J
imechanganuliwa zaidi na kuandikwa wakati sarufi ya lugha C ni mara chache
kuandikwa kwa vile huchukuliwa kuwa ni hafifu.
Mambo
yanayoweza kusababisha diglosia kutokea
a. Kuwepo lugha zaidi ya moja au
kutokea kwa lahaja nyingi katika lugha.
b. Kuwepo kwa matabaka katika
jamii. Tabaka lenye nguvu kisiasa, kiuchumi litaathiri uteuzi wa lugha J.
**Hadhi ya lugha, Mekacha
(2000:133) anaeleza kuwa, kupanga hadhi ya lugha huhusisha vi[pengele viwili
ambavyo ni uteuzi wa lugha au kilugha cha kutumika kama lugha rasmi na pili ni
utekelezaji wa mabadiliko yatakayowezesha watu kutambua, kukiri na kufuata
matumizi ya lugha yaliyokusudiwa. Aidha Haine (1992) anaeleza kuwa tunaposema
lugha fulani ina hadhi tuna maana kwamba lugha hiyo inamnufaisha mzungumzaji
kijamii, kiuchumi, kielimu, kikazi na kisiasa. Haine (keshatajwa) anataja sifa
za lugha zenye hadhi ya juu na sifa za lugha zenye hadhi ya chini kama
ifuatavyo;
Lugha
zenye hadhi ya juu
|
Lugha
zenye hadhi ya chini
|
i.
Zimesanifiwa na zinatumia lugha rasmi.
ii.
Nyingi ya lugha hizi zinatoka ulaya au nchi
zilizoendelea kiuchumi
iii.
Zinatumika kama lugha za kufundishia katika mfumo rasmi
wa elimu. Baadhi ya wazungumzaji hujifunza lugha hizi shuleni kama lugha ya
pili.
iv.
Zinakuzwa na kuendelezwa kwa kuwa na mipango madhubuti
iliyoandaliwa katika sera ya lugha.
v.
Ni rahisi mzungumzaji kupata kazi nzuri kwa kutumia
lugha hizi.
vi.
Zina historia ndefu ya karne nyingi zilizopita ya kuwa
na maandishi yaliyohifadhiwa ya lugha hizi.
vii.
Hutumiwa na watu wenye nafasi za juu serikalini katika
siasa, uchumi, elimu, dina na kadhalika.
|
i.
Hazikusanifiwa na zinatumia lugha lugha zisizo rasmi
yaani za kilahaja au kikanda.
ii.
Ni lugha ya kijadi
iii.
Inatumika katika mawasiliano ya kawaida
iv.
Zinatumika kama lugha za kufundishia katika mfumo usio
rasmi wa elimu. Baadhi ya wazungumzaji hujifunza lugha hizi majumbani au
mitaani kama lugha ya kwanza
v.
Hazina historia ndefu, kwakuwa haizikuwekwa katika
maandishi
vi.
Haina uhusiano wa moja kwa maoja na upataji wa ajira
hususan katika nchi ya Tanzania.
|
Triglosia
Triglosia hutokea kunapokuwa na lugha
moja kuwa na hadhi ya J na nyingine kuwa C lakini katikati ya lugha hizi
kunakuwa na lugha nyingine yenye nguvu kihadhi kuliko lugha C. mfano mahusiano
ya lugha ya Kiingereza, Kiswahili na lugha nyingine za kijamii kwa Tanzania
ambapo Kiswahili kina nafasi ya Kati. Uhusiano huu ni wa kidarajia.
Poliglosia
Poliglosia ni sawa na triglosia
isipokuwa tofauti yake ni kuwa katika poliglosia kunakuwa na lugha nyingi zenye
hadhi tofauti katikati. Mfano, Kiingereza, Kifaransa Kiswahili na Lugha za
kijamii kama Kihehe.
KUTOFAUTIANA
KWA LUGHA
Viwango
vya kutofautiana kiisimu katika lugha
(a) Mabadiliko
ya kifonetiki na kifonolojia
Katika hali halisi si rahisi
watu wote kuwa na matamshi sawa katika jamiilugha yote. Kwa vile hata mtu mmoja
hawezi kumudu matamshi yake sawa wakati wote kutokana na ulimi kuteleza, hali,
maumbile, nk. Katika kiwango cha jamii hutokea pia kuwa na namna ya matamshi
inayowatambulisha kama kundi moja. Mfano wameru, wachaga, wapemba, wamakonde
nk. Tofauti hizi hujidhihirisha katika sauti, toni, wakaa, lafudhi nk.
b)
Tofauti za mofolojia
Mabadiliko ya kimofolojia
huhusisha kuongezwa, kudondosha au kuungana kwa mofimu tofauti. Tukio hili
huweza kutokea kwa namna tofauti.
Kuongezwa kwa viambishi.
Lima>
limaga/halimagi, mjombae/mamaae[wameru]
Vilevile
kunakuwa na matumizi mabaya ya upatanishi wa kisarufi miongoni mwa wazungumzaji
wa lugha ya Kiswahili kutokana na athari ya lugha mbalimbali.
Mfano:
mbuzi yangu, funguo yangu, nyimbo yangu
Vilevile
neno moja laweza kupewa dhima ya kiambishi na hivyo kuambatanishwa na maneno
mengine. Katika
Kiswahili tuna mfano mzuri wa neno bongo. Bongoland,
bongostarsearch, bongo….
Ufananishaji au ubadilisho ni sababu nyingine ya kutokea kwa
tofauti za kimofolojia katika lugha. Ubadilisho hutokea wazungumzaji
wanapoongeza kiambishi fulani katika neno tofauti na kanuni za lugha husika
zinavyosema
Mfano: kaka> m-kaka>wakaka,
baba> m-baba
Huenda> kuenda-ga.
Haendi > haenda-gi.
Kiongozi > mkiongozi
Kiosk > Ki-oski> vi-oski
Video >vi-deo> Ki-deo
c)
Tofauti za kimsamiati
Ukopaji ni chanzo kikuu cha
mabadiliko ya kimsamiati kutokana na kuwa lugha huingiliana na kusababisha
ukopaji kutokea. Mfano, Kiswahili kimekopa asilimia 40 kutoka lugha mbalimbali
wakati Kiingereza kimekopa 60% kati ya msamiati wake unaoandikwa kutoka kilatini
na kigiriki, kutoka kifaransa na kutoka kifaransa kupitia kigiriki na kilatini.
Katika jamiilugha kunakuwa na
kundi la wazungumzaji wanaotumia maneno ya mkopo tuwaite wanamabadiliko mfano
wasomi na kundi lingine ni la watu wasiotumia maneno ya mkopo tuwaite
wasiopenda mabadiliko.
Muziki: Siingo, promota,
Soka: gemu, spoti, refarii,
kadi nyekundu/njano
Elimu: disco, kichwa, maksi,
somo
d)
Tofauti za kisintaksia
Lugha zinaweza kugawanywa
katika makundi kutegemeana na jinsi muundo wa sentensi unaozingatiwa. Kiima
(K), kitenzi (T) na yambwa (Y). Hivyo, tunaweza kupata lugha zenye KTY, KYT au
TKY. Kama ilivyo upande wa mabadiliko ya kifonolojia na kimofolojia, lugha
yaweza kubadilika kisintaksia kutoka aina moja hadi nyingine.
Kunaweza kutokea tofauti za
ndani ya lugha yenyewe ambapo watu wanapozungumza huanza kutumia muundo tofauti
na uliozoeleka.
Mfano: TK= anasema John.
Vilevile lugha yaweza kukopa
miundo kutoka katika lugha nyingine kupitia kikundi fulani cha wazungumzaji. Kwa mifano;
·
mabibi
na mabwana,
·
kwa
uchache,
·
mwisho
wa siku “at the end of the day”
·
Kwa
vyovyote “all in all”
·
Kile
kitabu ni change “ that book is mine”
·
Simama
juu “stand up” badala ya simama
·
nk.
e)
Tofauti ya kimaana
Maana za maneno zinaweza
kubadilika katika lugha kutokana na watu kutaka kuelezea hisia zao kwa namana
iliyo tofauti. Maana hizi hubadilika kutoka kundi moja hadi jingine. Mfano
vijana wanaweza kutumia neno fulani wakiwa na maana fulani tofauti na
ilivyozoeleka yaweza kubadilika katika sura tatu.
·
Kupanuliwa
kwa maana ya neno
·
Kufinywa
kwa maana ya neno
·
Maana
ya neno kuhama
Neno kupe, mwanga, bibi,
shangazi, bongo
LAFUDHI
NA REJESTA
a.
Lafudhi
Lafudhi
ni tofauti za
kimatamshi zinazojitokeza kwa watumiaji wa lugha moja. Hivyo, lufudhi hujikita
zaidi katika matamshi.
Kila mtu ana lafudhi yake kama ilivyo
kwa kila mtu kuwa na lahaja yake. Hii hutokana na ukweli kuwa mtu anaweza kutumia
lugha kwa namna tofauti kimatamshi kwa vile si rahisi kudhibiti matamshi yake.
Hivyo, inapofikia swala la lafudhi hoja si mtu kuwa au kutokuwa na lafudhi bali
ni lafudhi au lahaja ipi mtu anatumia.
Kwa mantiki hiyo,
tuna lafudhi ya mtu mwenyewe katika Kiswahili, Kiingereza katika kiswahili,
kilingala katika Kiswahili, kinyakyusa katika Kiswahili, kimeru katika
Kiswahili.
b.
Rejista
Watu wanapokuwa
katika muktadha fulani hulazimika kutumia lugha inayoendana na muktadha husika.
Mathalani, A anapokutana na rafiki yake wnayelingana kiumri watatumia lugha
iliyotofauti na wanatakapokutana na mtu mwenye umri tofauti. Vilevile A
atakapokuwa sokoni atalazimika kutumia lugha ya sokoni, akiwa kanisani au
msikitini atatumia lugha ya kanisani/msikiktini, akiwa mchezoni (lugha ya
mchezoni) akiwa safarini (safarini), mazungumzo au mandishi nk.
Chunguza mifano
ifuatayo:
·
Mimi
utumbo
·
Chukua
vichwa
·
Jamaa
anakamua kinoma
·
Umeanza
dakika ishirini zilizopita
Wazungumzaji hao wanatoka kundi
gani?
Hivyo, tunaweza
kusema rejista ni aina yoyote ya lugha ambayo inatumika katika muktadha fulani.
Katika mazingira
rasmi kunakuwa na matumiza ya lugha rasmi; uteuzi wa msamiati, sentensi
zinazofuata kanuni nk. Katika mazingira yasiyo rasmi kunakuwa na matumizi ya
lugha isiyo rasmi. Mfano, matumizi ya msamiati usio rasmi, sentensi zisizokuwa
rasmi, lugha inayobagua, udondoshaji wa msamiati au kifungu cha maneno, nk
Tunaweza kupata
mtindo wa matumizi ya lugha wa mahakamani, redioni, runinga, magazetini, shuleni/vyuoni,
michezoni, dini,sayansi, sanaa, biashara, mandishi, mazungumzo,
siasa,hosipitalini,jeshini, wapenzi wawili, wanarika, kikazi, vyombo vya usafiri nk. Mtu mmoja atalazimika
kutumia lugha kuendana na mazingira husika. Matumizi haya yaweza kuambatana na
matumizi ya istilahi au misimu.
Mtindo
Mtindo katika lugha hauna budi
kuuona kama dhana ambayo si rahisi kuitenganisha na lafudhi. Hii inatokana na
ukweli kuwa wakati mtindo huzungumzia namna ya kutumia lugha lafudhi
huzungumzia matokeo ya namna ya kutumia lugha yaani aina tofauti za matamshi ya
lugha tu. Mtindo unaenda mbali zaidi hadi kwenye mandishi, viungo, matamshi,
nk.
Mtindo wa utendaji unaweza kuwa
wa kirazini
ü
Kuteua
matumizi ya lugha kwa watu tofauti
ü Uteuzi
sahihi wa misemo, sentensi, nk
Mtindo pia waweza kuwa wa nusu
urazini
ü
Kutumia
lugha ya hisia kama ukali, huzuni, uchovu nk pasipokujua
ü
Kubadili
namna ya matamshi pila kujua
ü
Kubadili
msimbo pasipokutarajia
ü
Kutumia
viungo vya mwili bila kupanga
ü
Kutumia
lugha ya jinsia pasipokutarajia
PIJINI
NA KRIOLI
Makundi mawili ya Wazungumzaji
wa lugha tofauti wanapokutana pamoja kutokana na sababu mbalimbali (Mfano
biashara, vita, siasa nk) wanapohitaji kuwasiliana wanalazimika kutumia njia
tofauti ili kuondoa tatizo la mawasilano.
a. Lugha inayozungumzwa na kundi
la wazungumzaji wengi huwa na nguvu kiasi cha kulazimisha kundi la wachache
kujifunza lugha ya kundi la wengi. Mfano, mataifa mengi yalilazimika kujifunza
lugha ya Marekani yalipohamia marekani.
b. Makundi yote mfano mawili
kulazimika kutumia lugha ya tatu iliyo ngeni kwa wote. Mfano kingereza,
kifaransa, kireno nk.
c. Njia ya tatu ni ya kuamua
kusawazisha lugha zilizopo mfano A na B na kuunda lugha ya tatu. Lugha
inayoundwa inaitwa pijini.
PIJINI
Pijini ni lugha inayotokana na
makundi tofauti ya watu wanaotumia lugha tofauti kukutana pamoj na kunda lugha
iliyo tofauti na lugha mama za makundi husika. Lugha hii hutokana na makundi
husika kuamua kusawazisha tofauti zao za lugha katika viwango vyote yaani,
matamshi, msamiati, mofolojia, sintaksia na maana.
Pijini hutokea zaidi katika
maeneo ambayo makundi makubwa ya watu hukusanyika kutokana na shughuli
mbalimbali kama vile biashara, viwanda, vita, ukoloni, nk. Lugha yenye nguvu
zaidi kijamii ndiyo inayochangia sehemu kubwa ya msamiati kwa vile wazungumzaji
wake huchukuliwa kuwa lugha yao ina hadhi kubwa zaidi kiuchumi, kisiasa na
hivyo kuvutia wazungumzaji wengi zaidi kujifunza na sio kinyume chake. Mfano,
pijini ya Papua New Guinea ya Tok Pisin ambayo msamiati wake mwingi unatokana
na lugha ya Kiingereza.
Tok
Pasin Kiingereza maana
Dok dog mbwa
Pik big nguruwe
Painim find kutafuta
Hukim hook kuvua
Sekan shake hand patanisha watu
Mazingira
ya kutokea kwa pijini
a. Makundi yanayotumia lugha
tofauti kutokuwa tayari kujifunza lugha ya upande mwingine.
b. Mwajiri na mwajiriwa.
c. Uvamizi wa kivita/ ukoloni
mfano waingereza, wafaransa na waamerika kuvamia maeneo mbalimbali ya asia na
pasifiki katika karnr ya 20. Mfano kuna pijini za kijapani na Kiingereza,
Vietinamu na kifaransa (Toæy Boæy).
Licha ya sababu hizi sababu
zinazoripotiwa zaidi ni makundi makubwa kuhamia eneo moja kutokana na sababu za
ajira kama manamba, madini. Mfano pijini ya kihawaii na Kiingereza ambapo wote
waliajiriwa katika mashamba ya manamba katika karne ya 19. Vilevile kuna sababu
ya muktadha wa biashara.
KRIOLI
Neno krioli awali lilitumika
kumanisha watoto waliozaliwa katika makoloni. Linatokana na neno la
kihispaniola la criollo. Baadaye neno
hili lilipata maana ya ziada kumanisha lugha zilizotumiwa na watoto waliozaliwa
katika makoloni (Lugha ya krioli). Hivyo, krioli ni lugha inayotokana
Umuhimu
wa kujifunza lugha za pijini na krioli
a.
Kujua historia ya jamiilugha
Kuna uhusiano mkubwa kati ya
jamii na lugha kama ilivyo kwa lugha na utamaduni. Kwa matiki hii kujifunza
lugha za pijini na lahaja kunawawezesha wanaisimujamii kujua mambo mbalimbali
ya jamii inayotumia pijini na krioli.
Kupitia krioli na pijini tunaweza kufuatilia historia ya jamii husika kuwa
zimepitia katika nyakati gani. Mfano ukoloni, harakati za kudai uhuru, manamba,
vita, uhamiaji, njaa nk. Vilevile tunaweza kujua makundi yanayopatikana katika
jamii na historia yake.
b.
Chanzo cha data za isimujamii
Jamiilugha za pijini na krioli
ni chanzo muhimu sana cha data kwa watafitu wa isimu-jamii wanaotaka kuchunguza,
kuchambua na kufafanua mabadiliko ya lugha na kukua kwa ulumbi katika jamii.
vilevile husaidia kuelezea sababu za watu kubadili msimbo wanapozungumza. Data
zote hizi hupatikana natika lugha za pijini na krioli.
c.
Chanzo
cha watunga sera za lugha
Kwa sasa
lugha za pijini na krioli zinatumika sambamba na lugha nyingine zikiwemo
zilizosababisha kutokea kwake. Mfano, Kiingereza, kifaransa, kireno nk. Mfano,
Pijini ya Tok Pisin (Papua New Guinea), Pijini ya Kinigeria (Nigeria) na pijini
ya Fanakalo (A. Kusini) Hutumika pamoja na lugha nyingine. Hivyo, lugha za
Pijini na Krioli hutambulika kama lugha nyingine. Hivyo, kuna haja kwa watunga
sera kuzitambua lugha hizi kama ilivyo kwa lugha nyingine na hata kutubutu
kuzipangia maeneo ya matumizi. Hi itazifanya lugha hizi kuzidi kukua zaidi.
Matatizo ya lugha za Pijini na Krioli
a.
Kuzihusisha lugha za pijini na biashara za utumwa na
hivyo watu wengi kutokuwa tayari kujifunza au kutumia kama ilivyo kwa lugha
nyingine. Hata hivyo watetezi wa lugha wanaona kuwa hii si sababu ya msingi.
b.
Msamiati mkubwa wa lugha za pijini na krioli unatokana na
lugha za nje ya Afrika wakati watumiaji wengi wa lugha hzi wanatoka Afrika.
Hivyo, wanona kuendelea kutumia na kusanifisha lugha hizi na kama sawa na
kuendelea kuuenzi ukoloni. Hivyo watumiaji wa pijini wanalazimika kujifunza na
kutumia lugh nyingine za asili au za kigeni.
Napenda kila kitu.
ReplyDeleteUpo vizuri mkuu
ReplyDeleteAsante kwa elimu hii mungu awabariki
ReplyDeleteMnaweza nieleza tofauti kati ya lugha mame na jamii lugha
ReplyDeleteUko vizuri mkuu
DeleteHi
DeleteAstinemMobge Joel Wisdom https://wakelet.com/wake/xs7geA7pz6mX-HL7qZ6J2
ReplyDeletedionajssketim
Kazi nzuri
ReplyDeleteAhsnt kwa kazi mzur tuendelee kushirikisna
ReplyDeleteAhsante kwa Kazi nzuri mi naomba msaada katika kujua vigezo vinavyotumika katika kuteua na kutumia lugha moja na sio nyingne katika jamii yenye ulumbi
ReplyDelete