maana ya sintaksia,uhusiano wa sintaksia na matawi mengine,malengo ya sintaksia au isimu miundo, vipashio vya lugha ni vipi?,
TUKI
(1990) wanaeleza na wanafasili dhana hii ya sintaksia au isimu miundo kuwa ni
tawi la sarufi linaloshughulikia uchanganuzi wa mpangilio na uhusiano wa
vipashio katika kila sentensi.
Habwe na Karanja (2004) wanapambanua
dhana hiii ya “sintaksia ni utanzu wa isimu unaoshughulikia muundo wa sentensi
na elementi nyingine zinazounda sentensi kama vile kategoria za maneno, vikundi
na vishazi”
Radford
(1981) anasema isimu miundo au sintaksia ni taaluma inayojishughulisha na namna
maneno yanavyoweza kupangwa pamoja kutoa muundo wa sentensi. Radford anaangalia
jinsi neno moja linavyoweza kujihusisha na neno
lingine na kutathmini muundo uliosahihi.
Dhana ya sintaksia ni utanzu wa sarufi
unaojishughulisha na uchanganuzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na
uhusiano wa vipashio vyake.( Massamba na wenzake (2001)
Sintaksi (au sarufi miundo/muundo) ni tawi la isimu au taaluma ya sarufi
inayoshughulikia namna ambavyo vikundi vya maneno na sentensi mbalimbali
zinajengwa katika lugha. Hasa hushughulikia kanuni zinazotawala mfumo wa vipashio vya lugha.
Sarufi muundo hushughulikia kanuni zinazotawala mpangilio wa maneno katika
lugha husika ili kujenga (kuunda tungo yenye maana). Kipashio ni kipande cha
neno au kikundi cha maneno yanayotoa taarifa fulani katika lugha ya Kiswahili.
Kuna vipashio vitano - navyo ni: Mofimu -->
Neno --> --> Kirai --> Kishazi --> Sentensi. Katika namna ya kutaja
au kutumia vipashio, ngazi ya mofimu ni ndogo kuliko neno. Neno ni ndogo kuliko
Kirai. Kirai ni kidogo kuliko Kishazi. Kishazi ni kidogo kuliko Sentensi. Hivyo
basi mpangilio wake halisi huanza kwa ukubwa na kuja udogo.
Kwa
ujumla twaweza sema isimu miundo ni utanzu wa sarufi ama kiwango cha isimu
ambacho hujishughulisha na uchanganuzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi
na uhusiano wa vipashio vyake katika kutengeneza tungo yenye uarifishaji
kamili. Katika sintaksia kitu cha msingi sana kinachozingatiwa zaidi ni sheria,
kanuni, ambazo hufuatwa katika kuyapanga maneno ya lugha katika mfuatano
unaokubalika na wenye kuleta maana inayoeleweka. Palipo na lugha yoyote huwa na
utaratibu wake maalumu wa kupanga vipashio katika tungo au sentensi.Licha ya isimu miundo huchunguza uhusiano wa maneno
katika tungo na kubainisha jinsi maneno yanavyoweza kumiliki na kutawala
mengine.
MALENGO
YA ISIMU MIUNDO (SINTAKSIA)
(i)
Kuchunguza tungo zinazokubalika katika lugha fulani mahususi.
Kwa mfano:- (i)Mwanajamii hodari alizawadiwa na raisi
wetu.
(ii)Hodari
alizawadiwa mwanajamii na raisi wetu.
Katika
tungo mbili hizi tungo ya kwanza ndiyo inayo kubalika katika lugha ya
kiswahili.
(ii)
Kubainisha utaratibu wa kila lugha
,kama ambavyo vipashio vidogo
vinavyoshirikiana kuunda vipashio vikubwa.
Sentensi za
Kiswahili zina muundo wa mtenda + tendo na kitendwa. Huu ni muundo mkuu wa
sentensi za Kiswahili na lugha zingine za Kibantu. Viambajengo vinavyounda
sentensi katika lugha ya Kiswahili ni Neno, Kirai na Kishazi. Vipashio hivi
huungana na kuunda tungo yenye hadhi kubwa zaidi. Neno ni kipashio cha lugha
ambacho kina sifa zote za Kisemantiki, kisintaksia, kimofolojia na kifonolojia.
Kirai ni kipashio ambacho huweza kuwa neno moja au zaidi ambapo ndani yake
sharti kuwe na neno kuu
Kwa mfano:-
(a) S = KN + KT
(b)KN = N + V
Katika
ujenzi wa lugha kipashio fulani hujiongeza na kuunda vipashio vikubwa zaidi
katika lugha fulani ambayo huwa ni tofauti na mfumo wa lugha nyingine.
(c)
Kuangalia utoshelevu wa kanuni au kaida katika kategoria zifuatazo
Mifano
ni kama vile
·
utoshelevu wa kiuchunguzi
·
utoshelevu wa kiufafanuzi na
·
utoshelevu wa kiuteuzi.
VIPASHIO
VYA LUGHA
Sintaksia
au isimu miundo hujishughulisha na mpangilio wa vipashio katika lugha husika,
vifuatavyo ni vipashio vya lugha ya Kiswahili ambavyo kwa pamoja hujenga lugha.
Vipashio huweza kuwa ni maneno au mpangilio wa maneno unaotoa taarifa Fulani au
usiweze kutoa taarifa kamilifu.Kila kipashio huwa na uamilifu na maana fulani.
Vipashio hivyo hupishana kihadhi baadhi ni vidogo ambavyo ni mofu na neno pia vingine ni vikubwa ambavyo ni kirai na
kishazi. Hivyo ufuatao ni mpangilio wa vipashio vya lugha ya Kiswahili kuanzia
kipashio kidogo kwenda kipashio kikubwa kama ifuatavyo.
Mofu
Neno
Kirai
Kishazi
Sentensi
UHUSIANO BAINA YA SINTAKSIA NA
MATAWI MENGINE YA ISIMU
Katika
lugha ya Kiswahili kuna matawi manne ya isimu ambayo ni
·
mofolojia,
·
sintaksia, fonolojia na
·
semantiki.
Hivyo ufuatao ni uhusiano baina ya sintaksia
na matawi mengine ya isimu ambayo ni semantiki,
mofolojia na fonolojia kama ifuatavyo:-
(a)Sintaksia na Semantiki.
Richard na wenzake (1985) wanasema kuwa semantiki
ni stadi ya maana, hivyo maana
hushughulikiwa katika vitengo au viwango vyote vya lugha ikiwemo sintaksia ambayo
hujishughulisha na mpangilio wa vipashio wa vipashio katika lugha.
hushughulikiwa katika vitengo au viwango vyote vya lugha ikiwemo sintaksia ambayo
hujishughulisha na mpangilio wa vipashio wa vipashio katika lugha.
Kwa mtazamo huo wa jumla wa isimu,
maana ya semantiki yaweza kujengwa katika muonekano ufuatao. Semantiki ni tawi
la isimu au taaluma ya isimu ambayo hufuata kanuni na taratibu maalumu katika
kuchunguza na kuchambua maana katika lugha. Maana hizo zaweza kuwa katika
maneno, vifungu au sentensi, pia maana zinazoshugulikiwa ni
zote, ziwe za wazi au zilizojificha.
Kwa mfano:-
(a)Musa
analima shamba.
(b)Musa
shamba analima.
Sentensi
ya kwanza ina maana kwani imefuata
mpangilio sahihi wa maneno, lakini sentensi ya pili haina maana kwani haina
mpangilio sahihi wa maneno. Hivyo basi ili tungo iwe na maana ni lazima
mpangilio wa maneno katika tungo uwe sahihi.
(b) Sintaksia na mofolojia.
(i)
Rubanza (1996) anasema kuwa mofolojia ni taaluma inayoshughulikia vipashio vya
lugha katika kuunda maneno. Kipashio cha msingi katika uchambuzi wa kimofolojia ni neno ambalo ndilo hutumika kuunda darajia ya sintaksia . Mofolojia kutoka maneno ya Kigiriki morphe, umbo, na logos, neno) au sarufi maumbo ni tawi la isimu ambalo huchunguza maneno ya lugha fulani na aina zake za maneno, hasa upande wa upangaji wa mofimu mbalimbali zitumikazo kwa ajili ya kuunda maneno.Mambo ya maneno ni matokeo ya muunganiko wa fonimu mbalimbali ambazo pia huungana na kuunda - hatimaye na kuwa neno. kama
Fonimu ---> Silabi ---> Neno.lugha katika kuunda maneno. Kipashio cha msingi katika uchambuzi wa kimofolojia ni neno ambalo ndilo hutumika kuunda darajia ya sintaksia . Mofolojia kutoka maneno ya Kigiriki morphe, umbo, na logos, neno) au sarufi maumbo ni tawi la isimu ambalo huchunguza maneno ya lugha fulani na aina zake za maneno, hasa upande wa upangaji wa mofimu mbalimbali zitumikazo kwa ajili ya kuunda maneno.Mambo ya maneno ni matokeo ya muunganiko wa fonimu mbalimbali ambazo pia huungana na kuunda - hatimaye na kuwa neno. kama
(ii) Vile vile maumbo ya kimofolojia huathiri
vipengele vingine vya sintaksia.
Kwa mfano:-
(a) Mkulima
anapandisha kilima kikuuu.
(b) Wanyama wanasumbua
msituni.
Hapa mofimu “M” na “Wa” upande wa kiima
imeathiri utokeaji wa mofimu “a’ na “wa”
upande wa kiarifu.
upande wa kiarifu.
(iii)Pia
kanuni za mfuatano na mpangilio wa mofimu au viambishi ukifuatwa huunda maneno
katika
Smiundo ya kisintaksia. Kwa mfano:-
katika
Smiundo ya kisintaksia. Kwa mfano:-
(a)
Alipika= A-li-pik-a
(b) Anachapa=A-na-chap-a
(iv) Kipengele cha umoja na wingi katika
maumbo ya kimofolojia kinaathiri umbo
linalofuata jina na kuathiri muundo wa sentensi nzima. Kwa mfano:-
linalofuata jina na kuathiri muundo wa sentensi nzima. Kwa mfano:-
(a) Mwanajeshi alikuwa anakimbia.
(b) Wana walikuwa wanasoma
kwabidii darasani.
Hapa majina ya umoja na wingi
yanaathiri mpangilio mzima wa sentensi.Hivyo vipashio hivyo huathiriana katika
sensensi kwani kipashio cha kwanza hutegemea sana kipashio cha pili ama
huathiriana ili kuleta maana.
(c)
Sintaksia na Fonolojia.
Kwa
mujibu wa Massamba na wenzake (1996) wanapambanua kuwa fonolojia kama ni uchambuzi wa mfumo wa sauti katika
lugha fulani mahususi. Ni jinsi ambavyo vitamkwa au sauti ya lugha
zinavyoungana ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha. Hivyo kuungana
kwa vitamkwa ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha fulani kutegemea
mpangilio sahihi wa vitamkwa kwa kuwa neno ni kiwango cha msingi cha uchambuzi
katika sintaksia basi fonolojia ina uhusiano wa moja kwa moja na sintaksia.
Kwa mfano:-
(a) Anacheka= A-na-
chek-a
(b) Anaimba=A-na-imb-a
Kwa ujumla sintaksia ni tawi mojawapo la isimu lenye maauhusiano ya
moja kwa moja na matawi mengine kwani haliwezi kutenganishwa na vitengo vingine
vya lugha kutokana na uhusiano mkubwa uliopo baina ya vitengo hivi. Hutegemeana
na kukamilishana kwani matawi hayo hufanya kazi moja ndani ya isimu.Kwa kupitia
uhusika huo katika kukamilishana na kutegemeana hakuna ukamilifu wa tungo kama
kaida na sheria za kisarufi hazito weza zingatiwa kwa ujumla au miundo yake
haita weza zingatiwa.Matawi hayo hakuna lenye ubora zidi ya tawi jingine ila
hufanya kazi kama vidole vya mkono kila kidole huwa na kazi yake lakini katika
kufanya kazi kwake huegemeana. Kwa mfano, huwezi kupata mofolojia
(neno) bila kupitia ngazi ya fonolojia na pia huwezi kuwa na ngazi ya sintaksia
(sentensi/tungo) bila kupitia ngazi ya fonolojia na mofolojia lakini vitengo
vyote hivi hutawaliwa na kitengo cha semantika ili kuleta mawasiliano miongoni
mwa wazungumzaji.
TUKI (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu.
Dar es salaam: TUKI.
Rubanza, Y.I (1996). Mofolojia
ya Kiswahili. Dar es salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Massamba, D.P.B na wenzake (1999). Sarufi
Miundo ya Kiswahili Sanifu: Sekondari na Vyuo. Dar essalaam: TUKI.
Habwe, J na P. Karanja (2004). Misingi
ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.
shukran sana
ReplyDeleteHongera bila shaka mmebobea katika kiswahili,,,
ReplyDeleteSantee Kaz nzuri
ReplyDeleteAsante
ReplyDeleteHongeren sana
ReplyDeleteShukran
DeleteKazi nzuri,, nlikuwa naomba ufafanuzi mzuri wa vpashio vya kisntaksia....
ReplyDeleteKazi nzuri,, nlikuwa naomba ufafanuzi mzuri wa vpashio vya kisntaksia....
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteVizuri
ReplyDeleteKazi nzuri sana. Ila pia ningepende kuuliza hapa. tumejema kuwa vipashio ni kipande cha neno au kikundi cha maneno yanayotoa taarifa fulani katika lugha ya Kiswahili. Mbona tusisime Kipashio ni kipande cha neno au kikundi cha maneno kinachoweza kutoa taarifa za kisarufi katika lugh ya Kiswahili.
ReplyDeleteTukisema hivyo tunatambua kuwa kipashio ni kipande cha neno kwa sababu ni kipande cha kimofolojia na kikundi cha maneno ni sintaksia. Je Viapshio vys mofolojia ni vipi na vipashio vya sintaksia ni vipi ambavyo hujenga kipengele cha mofosintaksia.
Mulei
Kazi nzuri sana. Ila pia ningepende kuuliza hapa. tumejema kuwa vipashio ni kipande cha neno au kikundi cha maneno yanayotoa taarifa fulani katika lugha ya Kiswahili. Mbona tusisime Kipashio ni kipande cha neno au kikundi cha maneno kinachoweza kutoa taarifa za kisarufi katika lugh ya Kiswahili.
ReplyDeleteTukisema hivyo tunatambua kuwa kipashio ni kipande cha neno kwa sababu ni kipande cha kimofolojia na kikundi cha maneno ni sintaksia. Je Viapshio vys mofolojia ni vipi na vipashio vya sintaksia ni vipi ambavyo hujenga kipengele cha mofosintaksia.
Mulei
Excellent
ReplyDelete🙏
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeletenimeipenda kazi ayko
ReplyDeletemarejeleo vizuri ukikamilisha kazi ili nzuri zaidi
DeleteAsante
ReplyDeleteTofauti kati ya sintaksia na sarifi
ReplyDelete