Semantiki kama taaluma nyingine ina mahusiano na taauma nyingine kama ifuatavyo katika mchoro na hatimaye katika maelezo yanayo eleza vipengele mbalimbali vya lugha:-
SEMANTIKIKI NA MATAWI MENGINE YA
Kazi hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu, sehemu ya kwanza ni utangulizi, sehemu ya pili ni kiini cha kazi na sehemu ya tatu ni hitimisho la kazi kwa ujumla.
Sapir,(1921)ana fasili maana ya
lugha kwa kusema "Lugha ni mfumo ambao mwanadamu hujifunza ili autumie
kuwasilishia mawazo, maoni na mahitaji. Mfumo huu hutumia ishara ambazo
hutolewa kwa hiari"
Mgullu,R.S(1999) anasema "Lugha ni mfumo
wa mawasiliano ya mwanadamu ambao hutumia mpangilio maalumu wa sauti kuunda
vipashio vikubwa zaidi kwa mfano mofimu, maneno na sentensi" Pia anadai
kuwa lugha ni mfumo wowote wa mawasiliano ya watu kwa mfano lugha ya Kifaransa.
lugha ya Kihindi.
Kamusi ya
TUKI(1990)inasema,"Lugha ni mfumo wa sauti zinazotumiwa na watu wa jamii
fulani wenye utamaduni unaofanana ili kuwasiliana"
Kwa ujumla tunaweza kusema
kuwa lugha ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo zimekubaliwa na jamii ya watu
fulani ili zitumike katika kukidhi mawasiliano yao ya kila siku katika nyanja
mbalimbali za maisha mfano siasa, uchumi na utamaduni.
Semantiki ni taaluma katika isimu
ambayo hushughulikia maana ya maumbo au sentensi katika lugha. Taaluma hii
ilianza enzi za Aristotle na Plato ambao walizingatia zaidi sifa za maana,
katika kipindi hicho walitaka kujua sifa na tabia za maana. Leech (1981).
Habwe
na Karanja wakimnukuu Richard na Wenzake (1985) wanasema “Semantiki ni stadi ya
maana. Semantiki ni utanzu unaochunguza maana katika lugha ya mwandamu”.
Wanaendelea kusema semantiki hutafiti maana za fonimu, mofimu, maneno na tungo.
Hivyo kutokana na fasili hii maana hushughulikiwa katika vitengo au viwango
vyote vya lugha ambavyo ni fonolojia, mofolojia na sintaksia.
Hivyo
kwa ujumla Semantiki ni taaluma katika isimu ambayo hushughulikia maana
ya maumbo au sentensi katika lugha. Taaluma hii ilianza enzi za Aristotle na
Plato ambao walizingatia zaidi sifa za maana, katika kipindi hicho walitaka
kujua sifa na tabia za maana. Hii inamaanisha kwamba
semantiki hutalii maana katika vipashio vyote vya kiisimu katika viwango
vyote vya lugha yaani fonolojia, mofolojia
na sintakisia.
Semantiki kama taaluma nyingine ina mahusiano na taauma
nyingine kama ifuatavyo katika mcoro na hatimaye katika maelezo yanayo eleza
vipengele mbalimbali vya lugha:-
Mchoro kuonesha
mahusiano ya semantiki na vipengele vingine vya lugha kama
sintaksia,mofolojia na fonolojia.Kuwepo kwa semantiki katikati inamaana kwamba
tawi hili ni muhimili wa matawi mengine.
.. |
Sintaksia, ni utanzu wa sarufi unaojihusisha na uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipasho vyake. Utanzu huu huchunguza sheria au kanuni zinazofuatwa katika kuyapanga maneno ili yalete maana inayokubalika na kueleweka katika lugha husika, . Kwa mantiki hii, kwa kuwa semantiki hushughulikia viwango vyote vya lugha, basi hushughulikia pia kiwango cha sintaksia ambapo huangalia maana za tungo, kwani tungo lazima ikubalike kwa wazungumzaji pia tungo lazima ilete maana.
Kwa
mfano,
Pana
huimba vizuri akiwa mubashara
Mubashara
huimba vizuri akiwa pana.
Vizuri
huimba pana akiwa mubashara.
Katika
mifano hii sentensi (1) inampangilio sahihi katika lugha ya Kiswahili hivyo
inamaana na inawezesha mawasiliano, na sentesi zilizobaki hazijafuata mpangilio
sahihi wa kimuundo wa lugha ya Kiswahili
hivyo hazina maana na hazifanikishi mawasiliano. Hivyo semantiki ina uhusiano
na mofolojia.
pragmatiki kuwa ni uchunguzi wa
maana katika muktadha wa mazungumzo au maandishi na inavyofasiliwa na
msikilizaji au msomaji. Semantiki na pragmatiki ni matawi yanayoshughulikia
maana katika sentensi, semantiki inashughulikia maana za maneno na kuangalia
muundo wa vipashio katika sentensi na pragmatiki inashughulikia maana
inayohusisha muktadha. Pragmatiki inashughulikia maana isiyo ya msingi bali
maana inayotokana na muktadha husika.
Mfano: neno baba katika muktadha wa kimapenzi ni mvulana
wakati semantiki
inashughulika na maana ya msingi ambayo inatoa fasili kulingana na kitu
kinavyoonekana kwa mfano neno baba litafasiliwa kama ni mzazi wa kiume
ambaye lazima awe na umri zaidi ya miaka kumi na nane Mofolojia ni taaluma inayoshughulikia vipashio vya lugha katika kuunda maneno. Tawi hili la isimu huchunguzi na kuchambuzi wa maumbo ya maneno na jinsi maumbo hayo yanavyotumika katika lugha. Jukumu la neno husika katika sentensi hubainika vyema kulingana na uhusiano baina ya maneno mengine katika tungo. Maumbo ya kimofolojia huathiri vipengele vingine vya kisemantiki. Hivyo semantiki ina mahusiano na taaluma ya mofolojia kwa kuwa ili lugha iweze kueleweka lazima iwe na mpangilio na muundo mzuri wa vipashio vya sentensi ili kuleta maana katika mawasiliano.
inashughulika na maana ya msingi ambayo inatoa fasili kulingana na kitu
kinavyoonekana kwa mfano neno baba litafasiliwa kama ni mzazi wa kiume
ambaye lazima awe na umri zaidi ya miaka kumi na nane Mofolojia ni taaluma inayoshughulikia vipashio vya lugha katika kuunda maneno. Tawi hili la isimu huchunguzi na kuchambuzi wa maumbo ya maneno na jinsi maumbo hayo yanavyotumika katika lugha. Jukumu la neno husika katika sentensi hubainika vyema kulingana na uhusiano baina ya maneno mengine katika tungo. Maumbo ya kimofolojia huathiri vipengele vingine vya kisemantiki. Hivyo semantiki ina mahusiano na taaluma ya mofolojia kwa kuwa ili lugha iweze kueleweka lazima iwe na mpangilio na muundo mzuri wa vipashio vya sentensi ili kuleta maana katika mawasiliano.
Mfano: Mwalimu anaimba
Walimu wanaimba
Katika mfano huu katika
upande wa kiima kiambishi m kinaashiria umoja na wa inaashiri wingi, katika upande wa kiarifu viambishi a katika upande wa kiima vinaashiria nafsi ya
tatu umoja na wa vinaashiria nafsi ya tatu wingi, hivyo
maumbo ya maneno lazima yawe na maana.
Pamoja na Semantiki kuangalia maana ni dhahiri kuwa si taaluma pekee
inayochunguza maana, kuna taaluma zingine zinazojitofautisha na Semantiki
katika kuchunguza maana, miongoni mwa taaluma hizo ni,Semiolojia, Leksikolojia
na Leksikografia.
Kuna wataalamu mbalimbali wanaofasili dhana ya leksikolojia
kama kipengele kinachokaribiana na semantiki, baadhi yao ni;
Ullmann (1962) ambaye
anafasili leksikolojia kama ni tawi la isimu linaloshughulikia mofolojia na
maana ya maneno.
Doroszewksi (1973)
kama alivyonukuliwa na Mdee (2010) amefafanua leksikolojia kuwa ni tawi la
isimu linalochunguza etimolojia, maana na matumizi ya maneno. Hivyo basi leksikolojia
ni tawi la isimu linalochunguza maana, mofolojia, etimolojia na matumizi ya
maneno. Uhusiano wa semantiki na leksikolojia; taaluma zote zinashughulikia
maana za maneno, leksikolojia inashughulikia maana zinazopatikana kwenye kamusi
na mabadiliko ya maana za maneno kwa mfano neno mtoto maana msingi ni kiumbe
anayezaliwa na binadamu na maana nyingine ni mpenzi na semantiki huangalia
maana ya msingi kwa mfano neno mama ni mzazi wa kike.
Katika kuangalia dhana ya semiolojia Massamba (2004)
amefasili semiolojia kama taaluma ya kisayansi inayojishughulisha na uchunguzi
na uchanganuzi wa mifumo ya ishara mbalimbali ikiwa inazingatia zaidi uhusiano
baina ya kiwakilishi na kitajwa.
Ferdinand de Saussure
kama alivyonukuliwa na Morris (1971) amefasili semiolojia ni uhusiano kati ya
alama na kitu, jambo au hali ya kitu inavyowakilishwa, akaaendelea alama ni
kiashiria na kitu ni kiashiriwa. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya
kiashiria na kiashiriwa.
Charles (1934)
alishughulikia dhana ya semiotiki kwa kuunda tanzu tatu ambazo ni sintaksia,
Pragmatiki na semantiki. Sintaksia ni taaluma ya uhusiano kati ya ishara na
vitu/ vielezo jinsi vinavyotumika, pragmatiki ni taaluma ya uhusiano kati ya
mfumo wa ishara na mtumiaji wake na semantiki ni taaluma ya uhusiano kati ya
maana na ishara. Hivyo basi semiotiki ni taaluma inayoshughulikia maana za
ishara/ taswira.
Semiotiki
hushughulikia neno kama kiwakilishi (utajo) cha kile kitajwa pia hushughulikia
maana ya msingi. Hivyo semiotiki inaona maana inapatikana kupitia taswira.
Yaani kila taswira lazima inakuwa na maana inayowakilisha. Kwa mfano rangi
nyekundu duniani inaashiria upendo hivyo maana ya upendo iliyojitokeza
imetokana na taswira ya rangi hiyo
. Hivyo katika taaluma hii maana zote za maneno zimefumbatwa
katika alama. Ni dhahiri kwamba ingawa semiolojia na semantiki hushughukia
maana, semiolojia kwa kiasi kikubwa hujihusisha na alama za kitaswira na
vielezo kwa kiasi kidogo wakati semantiki huchunguza maana katika mfumo wa
ishara wa lugha inayozungumzwa na binadamu. Semantiki inatofautiana na
semiolojia kwani semantiki inashughulikia alama za lugha yaani kila lugha huwa
na alama zinazoashiria kitu fulani wakati alama za semiolojia hazihusu lugha
yaani huwa ni maana za mawasiliano, mfano ishara za mawingu, wanyama kama bundi
ishara ya uchawi.
Vilevile katika
kipengele hiki tunaona jinsi dhana ya leksikografia ilivyofafanulia, uhusiano
na semantiki.
Mdee (2010) anafasili leksikografia ni kazi ya kisanaa na
kisayansi ya kutunga kamusi ambayo hujumuisha uorodheshaji wa msamiati wa lugha
inayotungiwa kamusi pamoja na maelezo yenye kufafanua kila neno
lililoorodheshwa kadri ya mahitaji ya mtumiaji wa kamusi aliyelengwa. Semantiki
na leksikografia huchambua maana na sifa za neno na uhusiano wa kimaana wa
maneno yenye kuunda kikoa maana. Katika leksikografia maana za maneno
zinapatikana katika fasili ya leksimu. Hivyo leksikografia huangalia maana
inayopatikana kupitia fasili, pia taarifa mbalimbali zinazoingizwa katika
kamusi kama za etimolojia, maana/fasili, matamshi, taarifa za matumizi
humsaidia msomaji kupata maana ya leksimu.
Semantiki inahusiana na taaluma hizo kwani taaluma zote
zimejikita katika kuangalia maana ya lugha, ingawa kila taaluma inaangalia
maana hiyo kwa namna tofauti tofauti. Pia taaluma zote ni taaluma za lugha,
hivyo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuonesha jinsi gani lugha inavyojiumbia
maana kutokana na hali halisi iliyopo
Kwa
ujumla semantiki ni tawi la isimu kama matawi wengine ya isimu ambalo haliwezi
kujikamilisha lenyewe pasipo kuhusiana na matawi mengine ili kukamilisha
mawasiliano. Lakini semantiki inaweza kutofautiana na matawi mengine kwa kuanza
na tafsiri yake ambayo inajieleza na imetofautiana kabisa kidhima na matawi
mengine ambayo ni fonolojia, sintaksia, na mofolojia. Pia dhima zake hazifanani
na matawi mengine ya isimu. Fonolojia ni tawi la isimu ambalo
hujishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha,
huchunguza jinsi ambayo vitamkwa au sauti za lugha zinavyoungana ili kujenga
maneno yanayokubalika katika lugha ya mawasiliano. Ili lugha ya mawasiliano iwe
kamili ni dhahiri kwamba mpangilio wa sauti lazima uwe na maana ili kufikisha
ujumbe, hivyo semantiki inauhusiano mkubwa na fonolojia.
Mfano: Neno “UA”
linamaanisha sehemu ya mmea pana maalumu kwa kutoa mbegu na kuvutia wadudu kwa
ajili ya uchavushaji lakini ikibadiliswa vitamkwa na kuwa ‘au’ huleta maana
tofauti na maana ya awali.
MAREJEO
Habwe, J na P. Karanja
(2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix
Publishers Ltd.
Massamba P. B. D (2004) Kamusi ya
Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI
Massamba, D.P.B na
wenzake (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu: Sekondari na Vyuo. Dar
essalaam: TUKI.
Richmond H Thomason (2012). What is
semantics? Second version. Oxford press
Massamba (2004) anafasili dhana ya
semantiki kuwa ni taaluma ya isimu inayojishughulisha na uchunguzi na uchambuzi
wa maana za maneno na tungo katika lugha.
Mgullu,R.S(1999)Mtalaa wa
Isimu,Fonetiki,Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili, Nairobi Kenya, Longhorn
Publishers.
I have enjoyed and is really educative and beneficial
ReplyDeleteFafanua kwa hoja
Deleteyur mom
ReplyDeletetungo ni nini
ReplyDelete