notes za malenga wapya,uhakiki wa shairi la malenga wapya.
UHAKIKI WA MASHAIRI YA MALENGA WAPYA
\MWANDISHI: TAASISI
YA KISWAHILI, ZANZIBAR
WACHAPISHAJI: OXFORD UNIVERSITY PRESS
MWAKA: 2001
JINA LA KITABU
WACHAPISHAJI: OXFORD UNIVERSITY PRESS
MWAKA: 2001
JINA LA KITABU
Jina la kitabu linasadifu yaliyomo katika kitabu. Kwa upande wa maudhui mambo yanayoelezwa mengi yanaigusa jamii ya sasa. Masuala ya maadili, siasa, uchumi, ukombozi wa kiutamaduni changamoto na suluhisho ya matatizo yanayoikumba jamii yanaendana na wakati wa sasa. Hivyo upya wa malenga wapya ni kweli. Kifani pia Malenga wapya wameweka muundo na mtindo wa kisasa.
Malenga wapya ni kitabu
kichaozungumzia masuala mbalimbali ya kijami kama vile ukombozi wa mwanamke,
umuhimu wa kilimo, umhumimu wa kuondoa matatizo katika jamii, ukombozi wa
mwanamke, umuhimu wa kilimo na kadhalika.
MAUDHUI
A : DHAMIRA
1) Suala la uongozi bora na uwajibikaji
Suala la uongozi limejadiliwa katika pande zote mbili za
uongozi mzuri na uongozi mbaya. Waandishi wameonesha yote haya wakiwa na lengo
la kuikomboa jamii. Wamesisitiza kuhusu uongozi bora mfano katika shairi la “Payuka”
anawaasa viongozi kuwa watekelezaji wa yale wanayoyaahidi na sio kuwa
wapayukaji tu. Mfano ubeti wa pili anasema
“Kupayuka kwenu huko,
Mbona
tu kokoriko,
Sioni linalokuwa.”
Pia katika shairi la “Puuzo” anawakanya viongozi
wasiowajibika kutekeleza majukumu yao na kuacha uzembe. Anawaasa kujituma na
kufanya kazi kwa bidii kwani ni wajibu wao. Anasema katika ubeti wa kwanza
“Ofisini ukifika,
wajitia pirika,
Haja
unayoitaka mwenyewe tahangaika,
Wajifanya hawajali.”
2) Ukombozi wa kiuchumi
Mwandishi anaona kuwa ili jamii ikomboke kiuchumi yapo mambo
ya msingi kutekelezwa. Miongoni mwa mambo hayo ni kufanya kazi kwa bidii na
kuacha uvivu. Mfano katika shairi la “Charuka” tunaambiwa kuwa,
“Charuka baba haraka, na mfano kuonyesha, Charuka
upate vuka, mikondo hii maisha,
Charukeni kina kaka, na dada nawaamsha,
Basi tena kulegea, charuka chacha rukaka.”
Pia anakazia suala la kilimo kama ndio msingi wa kujikomboa
kichumi katika shairi la “Adui” na katika shairi la “Mkulima”anaonesha
umuhimu wa kumthamini mkulima na kilimo. Vikiwa kama vigezo vya maendeleo
nchini mwetu. Mfano katika shairi la “Adui” anasema;
“Tulime jama tulime, tushinde adui njaa, Hapa
kwetu ituhame, kwingine kutokomea,
Wala sisi tusikome, chakula kujilimi
Tutie jembe mpini, tuteremke shambani”.
Pia katika shairi la “Tuyazingatie haya” mwandishi
anataja mambo ambayo anaamini kuwa yakizingatiwa yataweka uchumi kuwa imara
kama vile, kuchapa kazi, kukomesha ubaguzi kutopora mali za serkali,
kushirikiana, kukosoana na kuepuka tamaa. Mfano ubeti wa pili anasema;
“Uchumi kuufufua, si hotuba refu sana, Moja
litalosaidia, ni kwa kuhamasishana,
Jengine
lafuatia, sote kushirikiana,
Tuyazingatie haya, wala tusirudi nyuma.”
3) Ukombozi wa mwanamke
Mwandishi kwa kutambua nafasi muhimu ya mwanamke katika
jamii, hakusita kuikumbusha jamii juu ya kuwaheshimu, kuwathamini, kuwapa uhuru
na kupinga tamaduni zote zinazomkandamiza mwanamke. Anaamini kuwa kumkandamiza
mwanamke ni kuikandamiza jamii. Anayazungumzia haya katika shairi la “Kifungo”,
“Hina inapapatuka”, “Raha”. Mfano katika shairi la “kifungo” ubeti
wa saba anasema;
“Kwa kuwa mwanamke, ndani mnanifutia,
Lazima nje nitoke,
kupata ninayotaka,
Nimechoshwa na upweke , sitaki kudhalilishika,
Kifungo
kimenichosha, minyororo nafungua.”
Pia katika shairi la “Hina inapapatuka”
anawahamasisha wanawake kukazana na kushikilia vipaumbele vya maendeleo,
anasema:
Nasaha ninatamka, mabibi nawaambia, Uzi
mulioshika, msije kuwaachia,
Ogopeni
kina kaka, yenu nkutowavunjia,
Unyonge inaondoa, hina inapapatuka”.
4) Suala maadili mema na maonyo
- Umuhimu Wa kuwa na kauli nzuri
Mwandishi katika shairi la “Ulimi” anawaasa watu kuwa ulimi
mzuri kwa maana ya kuongea vizuri na watu kwa adabu, na heshima. Anaona kuwa
ulimi ni kiungo kidogo lakini kinaweza kusababisha matatizo au mambo mazuri.
Anauasa ulimi akisema;
“Usiropokeropoke, kwa wenzio kwanza sema,
Usipachikepachike, maneno yasiyo mema,
Useme wanufaike kwa kauli yako njema,
Ewe
ulimi sikia!
- Umuhimu wa kutenda wema kwa binadamu wenzetu
Mwandishi anaona kuwa wanajamii wanapaswa kutenda wema kwa
wanajamii wenzao kwani matokeo ya wema ni mafanikio na shukrani. Anasema katika
shairi la “Hisani hulipwa”
“Akuulizae, uwapo na shida,
Akuteteae ukishambuliwa,
Akumurikae,
uwapo na giza,
Hisani hulipwa
- Umuhimu wa kuwa na subira katika maisha
Mwandishi anawaasa wanajamii kutokurupukia maisha hasa
vijana. Katika shairi la “Siharakie maisha” Anaona upo umuhimu wa
kufanya mambo kwa wakati na kuacha tamaa kwani kila jambo na wakati wake.
Anawaasa wanafunzi kushikilia masomo na kutolimbukia mambo ambayo si wakati
wake. Anasema; “Punguza
haraka zako,
Badilisha mwendo
wako,
Subira ni chombo chako, Takutwisha
kwenye fuko,
Usisahau
usemi, subira yavuta heri.”
- Umuhimu wa kuishi vyema duniani
Katika shairi la “Ulimwengu” na “Maisha ni kama
njia” mwandishi anaiambia jamii kuishi vizuri katika dunia kwani dunia ni
mapito tu. Mfano katika shairi la “Maisha ni kama njia” anasema:
“Iweze yako suduri, binadamu zingatia,
Kaa kutafakari, utende yalo sawia,
Ubabe au kiburi, havitokusaidia,
Maisha
ni kama njia, tukumbuke akhiria”.
Pia katika shairi la “Ulimwengu” mwandishi
anawaambia wanajamii kuwa katika dunia kuna mambo mengi mabaya na mazuri hivyo
ni budi kuyavumilia na kuendanana nayo vizuri. Anasema ubeti wa nne;
“Umbile vile lilivyo, ni umbo la mitihani,
Usilendeshe visivyo, litakupa hamkani,
Ambaa
hebu rudivyo, ulimwengu ni shetani,
Ulimwengu!
- Uaminifu katika ndoa
Suala la ndoa kwa jinsi anavyosema mwandishi uaminifu ndio
jambo la msingi kwani huleta upendo na amani kwa familia. Anawashauri wanaume
kujali familia zao na kuwa na mahusiano mengine nje ya ndoa. Katika shairi la “Kwanini”
anasema;
“Mke wake, atamwacha, singizini,
Atoroke, parakacha, migombani,
Kumbe kake, anakocha, mwa jirani,
Kwanini?”
Mume
pesa, apeleke, chumbageni,
Azitesa, toto zake, firauni,
Apepesa, mwendo wake, ulevini,
Kwanini”.
- Matumizi mazuri ya pesa
Mwandishi anaona upo umuhimu wa kutofuja pesa. Anashauri
watu kuwa na utamaduni wa kuweka akiba. Anaona kuwa ufujaji pesa ni dhambi na
si haki. Katika shairi la “Israfu”
“Mali ulojichumia,
Ni yako nakubalia,
Lakini
kiangalia,
Vipi unaitumia,
Mwenzangu nakuusia, israfu haifai.”
- Kuzingatia dini na kumuabudu Mungu
Mwandishi anawaasa wanadamu kutii maadili ya dini zao. Kwani
misingi ya dini huelekeza watu katika mema. Anasema haya katika shairi la “Maisha
ni kama njia”. Ubeti wa tano anasema;
“Tamati nawashauri, tumuabudu jalia
Ibada
na tukithiri, na kutenda yenye njia,
Twenda kila mahali shubiri, hukumu yatung
Maisha ni kama njia, tukumbuke akhiria”
5) Suala la Mapenzi
Katika shairi la “Ua” na katika shairi la “Nipate
wapi mwingine” waandishi wanaona kuwa mapenzi ya dhati na ya kweli ni jambo
jema. Anawataka watu kuthamini na kuwaheshimu wapenzi wao na binadamu wengine.
Mfano katika shairi la “Ua” anasema;
“Ua limejituliza, mtini laning’inia, Mwenyewe
laniliwaza, furahani laniti
Ua sasa limepea, macho walikodolea.”
Pia katika shairi la “Nipate wapi mwingine” mwandishi
anazungumzia jinsi ilivyo kazi kupata mpenzi wa kweli. Dunia sasa imebadilika
watu hupenda vitu vingine badala ya kuwa na mapenzi ya kweli yanayojali utu wa
mtu. Mwandishi anayaita kuwa hayo ni mapenzi ya ulaghai. Mashairi ya “Utanikumbuka”
linaasa juu ya usaliti katika mapenzi kuwa haufai. Shairi la “Kuunge” na
“kitendawili” yanakazia zaidi juu ya kuwa na msimamo katika mapenzi.
Anafananisha watu wasio na mapenzi ya kweli na Njiwa anayerukaruka asiyetulia.
Mwandishi anasema;
“Wapo wafugaji tele, madebe wamepachika,
Na njiwa wapo milele, watu hawendi kutaka,
Kutwa waweka kelele, wapanda mara kushuka,
Njiwa ameshanitoka,
nipate wapi mwingine”.
Mwandishi anayaita kuwa hayo ni mapenzi ya ulaghai
6) Umuhimu wa wosia
Suala la kutoa wosia kwa mwanadamu ni jambo la muhimu sana
pindi anapokufa. Suala hili huepusha migogoro na malumbano kwa wanafamilia
wanaobaki. Katika shairi la “Nini wanangu” anasema:
“Shikamaneni wanangu, siku yangu ikifika.
Mutamakani kichungu, musije kutawanyika, Kiondoeni
kizungu, mshike mliposhika,
Sizidi nasaha zangu!”.
7) Suala la ukombozi wa kifikra
Mwandishi anaitaka jamii kukomboka kifikra. Mambo haya
anayazungumzia katika shairi la “Usiwe bendera”. Suala la kuwa na
msimamo binafsi na thabiti katika maamuzi ya mambo ni jambo la msingi katika
maisha ya kila siku. Anaona kuna athari ya kuendeshwa au kuamuliwa mambo kama
bendera inavofuata upepo. Mfano;
“Tumia zako fikrazo, pima yanofaa, Tazama
kikwazo, wapi chatokea,
Pima na uwezo, wakukifanyia,
Usiwe bendera, kufata upepo”.
8) Utetezi wa haki
Mashairi ya “Mpaka lini”, “Samaki mtungoni” “Sokomoko”
yanazungumzia juu ya ukosefu wa haki. Mahali popote hapawezi kuwa na amani bila
kuwepo haki. Hivyo mwandishi anaeleza:
“Msema kweli, kwenu ninyi ni chagizo,
Mtaka
hali, havuki mbele ya vikwazo,
Mwongo sana, kwenu ninyi ni kigezo, Mpaka
lini mtatuchezea?”
Katika shairi la “Samaki mtungoni” mwandishi anaona
kuwa kwa sababu ya ukosefu wa haki watu hudhulumiwa na kuteswa anafananisha
wadhulumu haki na wavuvi anasema:
“Haki yao mepotea, na heshima kuondoka,
Mebaki waning’inia, mtungoni mepangika,
Bwana amechachamaa,nyumbani
kwenda kupika,
Leo
wako mtungoni, huzuni imewakumba.
9) Utabaka na unyonyaji na unyanyaswaji
Mambo ya matabaka ndiyo yanayochangia kunyanyaswa, kunyonywa
na kukandamizwa. Matabaka ambayo waandishi wanayazungumiza ni matabaka ya
kiuchumi, kijamii na kisisasa. Katika shairi la “Samaki mtungoni” samaki
anachorwa kama mtu mnyonge na mvuvi akiwa ni mwenye mabavu. Anaonesha jinsi
watu wasivokuwa na uhuru bali kukandamizwa na kuteswa. Hili limewekwa wazi ili
kupiga vita mambo hayo katika jami. Anasema:
“Huzuni imewakumba, raha zao
kutoweka,
Mvuvi amewasomba, mtungoni
kuwaweka, Hakuna wa kumuomba, msamaha kuutaka,
Leo wako mtungoni huzuni imewakumba.”
Pia katika shairi la “Bahari” mwandishi anawapiga
vita viongozi na watawala wanaowanyanyasa wananchi wenzao.
“Hudai ni haki yao, mola amewajaalia,
Kuwadhulumu
wenzao,
wao Nao kwa unyonge wao, wadogo wateketea, Bahari
ina hatari, wala usiichezee.”
Vilevile katika shairi la “Punda” mwandishi anaelezea
jinsi ambavyo watu wa hali ya chini wanavyoendelea kuonewa na kuteswa kama
Punda. Anaishauri jamii kukemea suala hili na kusaidiana kuwainua wanyonge na
sio kuendelea kuwanyonya.
“Toka ulipozaliwa, maishayo ni kizogo,
Hujapata kuenziwa,
waishi trigivyogo,
Nawe hujajielewa, u kiumbe hu kigo
Kama
ungefadhiliwa usingebeba mizigo
Hakika ulionewa hustahili kipigo, Haki
umeitambua, idadi japo kidogo”.
B; FALSAFA
Falsafa ya waandishi wa mashairi ya “Malenga wapya” ni kuwa
jamii inaweza kubadilika kiuchumi na kupata maendeleo kama itafanya kazi kwa
bidii bila kuzembea, wanaamini kupingwa kwa utabaka na unyonyaji ni suluhu ya
amani na maendeleo. Wanaamini pia ukiishi vizuri duniani utafanikiwa,
wanasisitiza kutenda wema. Haki usawa na ushirikiano ni chachu ya maendeleo.
C; MTAZAMO
Mtazamo wa waandishi ni wa kiyakinifu kwani mambo
wanayoyaeleza kama vile namna ya kutatua matatizo katika jamii. Mambo
wanayoyapendekeza yanawezekana kutimizika mfano uwepo wa haki, kupinga utabaka,
unyonyaji, kufanya kazi vizuri kuweka akiba na matumizi mazuri ya pesa na mambo
mengine mengi.
D; MSIMAMO
Msimamo wa kimapinduzi ni msimamo wa waandishi wa
diwani hii. Mambo wanayoyaeleza yanalenga kuleta mapinduzi katika jamii mfano
kupiga vita adui uvivu, kupinga dhuluma, kupinga maovu yote. Hiyo ni ishara
kuwa wanalenga kuibadilisha jamii. Wanatoa pia changamoto na suluhu ya matatizo
katika utekelezaji wa mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika jamii kama
vile kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili.
E ; UJUMBE
- Kufanya kazi kwa bidii ni chachu ya mendeleo
- Uaminifu katika ndoa, mapenzi ya kweli ni jambo la msingi
- Matumizi mazuri ya pesa husaidia kuwa na akiba nzuri na kupunguza umaskini
- Kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi, si budi kukithamini
- Kauli nzuri huepusha migogoro na chuki
- Kumkomboa mwanamke ni kuikomboa jamii, hivyo si budi kupinga tamaduni zinazomkandamiza
- Tunaaswa kupinga utabaka. Kutetea haki na kupuuza unyonyaji ili kuleta usawa katika maisha
- Viongozi walaghai na wasaliti hawafai kwa maendeleo hivyo tunaaswa kuwa makini kuchagua viongozi bora na kuwawajibisha
- wasiofaa.
Maswali ya mazoezi
1. Maadili mema na maonyo yamejadiliwa na washairi wa
diwani. Onesha mjadala huo kwa kutumia diwani mbili.
2. Ni kwa vipi muundo na mtindo wa ushairi hutofautiana na muundo wa riwaya na tamthilya? Tetea jibu lako kwa kuonesha jinsi muundo na mtindo wa ushairi ulivyo.
3. Ujenzi wa taswira katika kazi za kifasihi hutufanya tuhisi au kuona kabisa uhalisia wa mambo ulivyo. Jadili kwa kutumia diwani mbili ulizosoma.
4. Waandishi wa kazi za fasihi ni walimu? Jadili.
5. Mtazamo, msimamo na falsafa ya mwandishi hututhibitishia ukweli wa mawazo yake katika kazi yake. Fafanua.
2. Ni kwa vipi muundo na mtindo wa ushairi hutofautiana na muundo wa riwaya na tamthilya? Tetea jibu lako kwa kuonesha jinsi muundo na mtindo wa ushairi ulivyo.
3. Ujenzi wa taswira katika kazi za kifasihi hutufanya tuhisi au kuona kabisa uhalisia wa mambo ulivyo. Jadili kwa kutumia diwani mbili ulizosoma.
4. Waandishi wa kazi za fasihi ni walimu? Jadili.
5. Mtazamo, msimamo na falsafa ya mwandishi hututhibitishia ukweli wa mawazo yake katika kazi yake. Fafanua.
Amaizing
ReplyDeletegood
ReplyDeletembona hamnamatumizi ya lugha
DeleteMbona mashairi hayajatengwa
ReplyDeleteTaswira ya mwandishi katika diwani ya malenga wapya zilizotumika Na maanii kuwasilisha ujumbe katika jamii
ReplyDeleteTaswira zielezwe vizuri peke yake
ReplyDeleteNi nzuri sana
ReplyDeleteIt's good tape for more
ReplyDeleteMbona hamja weka fan ni maudhui peke yake 2 ndo nimeona apa kwny page yenu
ReplyDeleteWakuu kuna maswali hapa naombeni msaada
ReplyDelete1: ujenzi wa taswira ni kipengele muhimu sana katik kupambanua lugha ya ushairi na kufikisha ujumbe kwa jamii. Jadil ukweli wa kaul hi kwa kutumia malenga wapya na cheka cheka
2: fan n muhmu sana katk kuifany kaz ya fash ikubalike kuw kaz ya sanaa chagua vtabu vwil ulvyosom kujadl kaul hii... Apo nipen msaad hata wa point 6 kla swal wakuu
Mbn hamjaelezea taswira vzr
ReplyDelete