isimu linganishi ,kazi ya isimu linganishi,majukumu ya isimu linganishi.
Katika kazi hii
tumejadili dhana ya isimu linganishi kwa kuangalia maana ya isimu linganishi
kama ilivyoelezwa wataalam mbalimbali,
malengo yake na jinsi inavyofanya kazi katika kulinganisha lugha.
Matinde, ( 2012),
anaeleza kuwa isimu linganishi ni tawi la isimu linalochunguza na kuchanganua
usuli na uhusiano uliopo kati ya lugha mbalimbali.
Massamba, (2009),
anaeleza kuwa isimu linganishi ni taaluma ya isimu ambayo lengo lake hasa ni
kujaribu kuonesha sifa bia za lugha mbalimbali au familia mbalimbali za lugha.
Wanjara, (2011),
anafafanua maana ya isimu linganishi kwa
kueleza kuwa ni tawi la isimu linalofanya uchanganuzi wa lugha mbili au zaidi
ili kuzilinganisha na kuzilinganua.
Hivyo, isimu linganishi
ni tawi la isimu ambalo lengo lake mahususi ni kufanya uchunguzi wa lugha
mbalimbali ili kuweza kuzilinganisha na kuzilinganua, ili kuonesha kufanana na
kutofautiana kwa vipengele mbalimbali vya lugha hizo na kuziweka lugha hizo
katika makundi kutegemeana na uhusiano wake.
Malengo ya isimu
linganishi ni haya yafuatayo :
·
kuchunguza mfanano na muachano wa lugha
mbili au zaidi
·
Hulinganisha na kulinganua vipashio
mbalimbali vya lugha mbalimbali ili kudhihirisha kufanana au kutofautiana kati
ya ligha hizo.
·
Isimu linganishi huchunguza lugha katika
viwango vyote yaani fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki ili kuonesha
na kueleza jinsi lugha hizo zinavyofanana na kutofautiana.
·
Kubainisha makundi mbalimbali ya
lugha kwa mfano familia za lugha kama
vile lugha ya kihindi , kizungu na lugha za kiafrika.
·
Kubainisha lugha zilizo na uhusiano
kinasaba na kuonesha jinsi lugha hizo zinavyotofautiana.
·
Isimu linganishi pia huangalia kufanana
na kutofautiana kwa namna lugha mbalimbali huunda maneno yake katika kurejerea
hali mbalimbali. Mfano lugha ya kilatini na kiingereza hubadilisha umbo la neno
kudhihirisha hali mbalimbali mfano kitenzi “do” hubadilika na kuwa “did” na
“done” kurejelea wakati uliopita.
·
Isimu linganishi pia hushughulikia
uchunguzi wa ukuaji wa lugha kwa mujibu wa mpito wa wakati.
·
Isimu linganishi hubainisha makundi
mbalimbali ya lugha na hata kufanikiwa kuunda lugha mama ya lugha husika kama
kibantu.
·
Isimu linganishi hujihusisha na
uainishaji wa lugha mbalimbali kwa mujibu wa vigezo anuai kama vile miundo ya
maneno, sentensi na ukuruba wa kihistoria. (Wanjara, 2011).
Tawi
hili la isimu linganishi hujikita katikabkuangalia jinsi lugha za binadamu
zinavyofanana kutokana na vipengele mbalimbali
vya kiisimu. Vipengele hivyo ni hivi vifuatavyo:
Lugha
hufanana kutokana na kuwa katika asili moja, Lugha za kibantu zinafanana kwasababu
zinatokana na lugha mame moja. Tukiangalia kufanana kwa lugha za kibantu katika
kigezo cha kiisimu vipengele vinavyoangaliwa ni kufanana kwa msamiati, muundo
wa kifonolojia, muundo wa kimofolojia, muundo wa kisintaksia na mpangilio wa
ngeli za majina. (Mgullu,2012)
Katika
kipengele cha msamiati pia tunaona kwamba msamiati wa msingi wa lugha za kibantu
na Kiswahili hufanana kwa kiasi kikubwa mfano,
Kiswahili kinyakyusa kinyiha kipogoro Kindari
Maji
amisi aminzi
Machi Amishi
Jicho iliso Ilyinso Lisu Ilyiso
Munyu umunyu umunyu munyu Umunyu
Kwa
mifano hiyo tunaona kuwa mizizi inafanana kwa kiasi kikubwa. Hivyo kuna
uhusiano wa kinasaba kati ya Kiswahili na lugha za kibantu.
Kufanana
kimofolojia, lugha za kibantu na Kiswahili zinafanana kwa kiasi kikubwa katika
mfumo wa maumbo ya maneno. Mfano namna viambishi vinavyopachikwa katika mzizi
wa maneno hufuata kanuni ileile kama inavyotumika katika lugha ya Kiswahili
yaani viambishi vinaweza kupachikwa kabla au baada ya mzizi na huwa na uamilifu
bayana.(Matinde,2012).
Kiswahili Kisukuma Kinyiha Kinyakyusa
A-na-lim-a A-le-lem-a A-ku-lim-a I-ku-lim-a
A-na
-chek-a A-le-sek-a A-ku-she-a I-ku-sek-a
Kutokana
na mifano hii tunaona kuwa kutenganisha viambishi hufuata kanuni mojakwamba
mahali palipo na kiambishi cha njeo mfano na-le (kisukuma) utaona kuna unasaba
baina ya lugha hizi.
Pia
kufanana kwa maumbo kati ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu kunaonekana
katika kuonesha idadi, ambapo viambishi huongezwa mwanzoni mwa kitenzi katika
lugha za kibantu na Kiswahili. Mfano:
Kiswahili Kinyakyusa Kisukuma Kinyiha
Wanalima bhikulima bhalelema bhakulima
Analia ikulila Alelele Akulila
Kutokana
na mifano hii tunaona kuwa lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu zinafanana
kwa sababu hata katika kuonesha maumbo ya umoja na wingi zote huongeza
viambishi mwanzoni mwa mzizi wa neno.
Pia
sintaksia ya lugha ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu hufanana kwa kiasi
kikubwa. Mfano jinsi ya mpangilio wa vipashio vyake na kuunda sentensi
hufanana, yaani mpangilio wa maneno hufuata kanuni maalum ambazo hufanana
katika Kiswahili na lugha za kibantu. Katika Kiswahili, sentensi inakuwa na
pande mbili yaani kiima na kiarifu, katika kiima kipashio kikuu ni nomino na
kiarifu kipashio kikuu ni kitenzi. Mfano:
Kiswahili - Mama anakula
Kihehe - Mama ilya
Kinyakyusa-
Mama ikulya
Kindali - mama akulya
Hivyo
muundo wa kiima na kiarifu wa lugha za kibantu unafanana sana na muundo wa
Kiswahili.
Mfumo
wa sauti (fonolojia) wa lugha za kibantu
unafanana sana na mfumo wa kiswahili yaani mpangilio wa sauti katika
kuunda silabi na miundo ya silabi. Mfano katika lugha ya Kiswahili hakuna
muundo wa silabi funge, muundo asilia wa silabi za Kiswahili huishia na irabu
pia hata katika lugha za kibantu silabi huishi na irabu. Mfano:
Kiswahili -
baba (k+I+K+I)
Kikurya -
Tata (K+I+K+I)
Kiha -
Data (K+I+K+I)
Kipare -
Vava (K+I+K+I)
Kinyakyusa- Tata
(K+I+K+I)
Kutokana
na mifano hiyo tunaona kwamba mifumo ya sauti katika lugha za kibantu hufanana
na mfumo wa sauti wa kiswahili. Hivyo lugha hizi ni za familia moja.
Mfumo
wa ngeli za majina katika lugha ya Kiswahili hufanana na mfumo wa lugha za
kibantu, hususani upachikwaji wa maumbo ya umoja na wingi na maumbo ya
upatanisho wa kisarufi. Katika lugha ya Kiswahili viambishi vya umoja na wingi
hupachikwa mwanzoni kabla ya mzizi wa neno, pia hali hujitokeza hata katika
lugha za kibantu. Mfano.
UMOJA WINGI
Kiswahili: M-tu wa-tu
Kinyakyusa: Mu-ndu Bha-ndu
Kinyiha: Umu-ntu Abha-ntu
Kikurya: Mo-nto Abha-nto
Kiha:
Umu-ntu abha-ntu
Kujitokeza
kwa vipashio vya umoja na wingi kabla na baada ya mzizi wa neno ni dhahiri kuwa
lugha hizi zinatokana na nasaba moja.
Pia
lugha hizi hufanana katika upatanisho wa kisarufi, lugha za kibantu na
Kiswahili huelekea kufanana viambishi vya upatanisho wa kisarufi hususani
viambishi vya nafsi ambapo huanzia na silabi. Mfano:
Kiswahili - Mtoto a-nalia
Kindali - Umwana a-kulila
Kisukuma - Ng’wana a-lelela
Kinyakyusa - Umwana i-kulila
Hivyo tunaona kuwa
katika lugha za kibantu na lugha ya Kiswahili viambishi vya upatanisho wa
kisarufi hutokea mwanzoni mwa kitenzi ambavyo vyaweza kuwa konsonanti au irabu.
Katika mifano hiyo hapo juu vimeanza na irabu, ambapo tunaona irabu “a” katika lugha za Kiswahili, kindali na
kisukuma na irabu “I” katika lugha ya kinyakyusa.
Pia lugha za kibantu na
lugha ya Kiswahili ni za asili moja kutokana na kufanana katika uainishaji wa
miundo ya maneno , Lugha za kibantu na Kiswahili zote ni lugha ambishi kutokana
na kwamba maneno yake hususan vitenzi huundwa kwa kuambisha mofimu kwenye mzizi
na kila mofimu ikiwa inawakilisha dhana maalum.(Wanjala, 2011).
Mfano;
Kiswahili: Anaimba a-na-imb-a
-a- Nafsi
ya tatu umoja
-na-
kiambishi cha wakati, kuonesha wakati uliopo
-imb-
Mzizi wa kitenzi
-a- kiambishi tamati
Kinyakyusa: Ikwimba
-i-kwi-mb-a
-i- nafsi ya tatu umoja
-kwi- kiambishi cha wakati kuonesha wakati uliopo
-mb- mzizi wa kitenzi
-a- kiambishi tamati
Kihehe: Alivemba
-a-kwi-mb-a
-a- nafsi ya tatu umoja
-kwi- kiambishi cha njeo kuonesha wakati uliopo
-mb- mzizi
-a- kiambishi tamati
Pia Wanjala (2011)
anaeleza kuwa ufanano wa lugha unaweza kujitokeza kwa bahati. Ambapo tunaona
kuwa kuna maneno yanafanana katika utamkaji katika lugha mbili ambazo si za
asili moja. Mfano :
Kiswahili Kiingereza
Makini Keen
Kata cut
Lugha pia huweza
kufanana kutokana na maingiliano ya kiisimu ya muda mrefu. Maingiliano haya
hupelekea lugha moja kuchukua maneno ya lugha nyingine ambayo ina muingiliano
nayo ya karibu. Mfano lugha nyingi za kibantu zilikopa maneno kutoka lugha za
kigeni wakati wa ukoloni. Mfano:
Kiingereza Kinyakyusa Kindari
Spoon supuni supuni
Church Kyariki Chariki
School sukuru Sukuru
Pia, hata lugha ya
Kiswahili ilikopa maneno mengi kutoka katika lugha ya kiarabu, kireno na
kihindi kutokana na muingiliano wa muda mrefu kipindi cha ukoloni, hali hii
imepelekea kuwepo kwa msamiati wa kiswahili unaofanana na msamiati wa lugha za
kigemi.
Mfano:
Kiarabu Kiswahili
Shukran Shukrani
Ahsante Ahsante
Akhera Akhera
Kihindi Kiswahili
Gari Gari
Laki laki
Lakini Lakini
Kireno Kiswahili
Leso Leso
Meza Meza
Nanasi Nanasi
Isimu jamii pia
hujikita katika kuangalia muachano wa lugha mbili au zaidi ambapo mambo
yanayopelekea lugha kutofautiana ni hizi zifuatazo.
Lugha kutokuwa katika
asili moja, lugha huweza kutofautiana kutokana na kutotokana na asili
moja.Mfano tunaona kwamba richa ya kuwa lugha ya kinyakyusa na kiiraki zote
zinapatikana Tanzania lakini lugha hizi mbili hazifanani kabisa katika
vipengele vyake mbalimbali kutokana na kwamba lugha hizi si za asili moja.(wanjara,2012).
Mfano:
Umbali wa kijiografia
huweza kupelekea lugha kutofautiana, Mwanaisimu linganishi anapotafuta sababu
ya lugha kutofautiana katika vipengele mbalimbali vya kiisimu huangalia pia
kigezo cha umbali, ambapo hali hii hupelekea lugha hizi kukosa muingiliano na
kusababisha kuwepo tofauti kubwa katika lugha hizo.Mfano lugha ya Kiswahili na
kiingerza zinatofautiana sana katika vipengele vya kiisimu kutokana na umbali
wa kijiografia, tofauti hizo ni hizi zifuatazo:
Katika uainishaji wa
ngeli za majina katika kuonesha umoja na wingi Kiswahili huweka viambishi
mwanzoni mwa nomino mfano:
Umoja wingi
Mototo
watoto
Chungwa machungwa
Darasa madarasa
Lakini katika
kiingereza idadi huweza kuoneshwa kwa njia tofauti tofauti kunaweza kuwa na mpangilio ulio
maalum au ule usio maalum mfano nomino child iliyo katika umoja, katika wingi
ni children, nomino book katika umoja katika wingi huwa books.
I like this
ReplyDeleteVery clear
ReplyDeleteGood job
ReplyDelete